Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha ameitaka timu ya kupambana na magonjwa ya mlipuko kushiriki kikamilifu katika zoezi la majaribio ya namna watakavyokabiliana na magonjwa hayo hasa maeneo ya mipakani.
Ameyasema hayo alipokuwa akifungua kikao cha kutambulisha zoezi la jaribio la namna yakukabiliana na magonjwa ya mlipuko katika wilaya ya Longido hususani eneo la mpaka wa Namanga na nchi jirani ya Kenya.
Amesisitiza zaidi kuwa zoezi hili nila muhimu sana kwa nchi hizi mbili kwani katika mipaka hiyo ni lango kubwa la wageni wengi kuingi na kutoka na hii itasaidi kuweza kupata uzoefu wakutosha wa namna ya kukabiliana na magonjwa hayo pindi yatakapotokea.
Akitoa maelezo mafupi ya zoezi hili mratibu wa magonjwa ya milipuko kutoka wizara ya afya,Jinsia, Wazee na Watoto Dokta Emmanuel Swai, amesema lengo kubwa la zoezi hilo linalotarajiwa kuanza Juni 11 hadi 14,2019 ni kuziimarisha timu hizo mbili za Tanzania na Kenya katika kukabiliana na magojwa hayo.
Pia,zoezi hili litasaidia kuchambua na kuainisha mapungufu ya mifumo ya miongozo na sheria ambazo hazitakuwa vizuri kulingana na mzingira ya sasa ya ufanyaji kazi. Amesema zoezi hili litafanyika katika maeneo ya mpaka wa Namanga (Kituo cha Forodha) na viwanja vya ndege vya Kilimanjaro na Jomo Kenyata na katika maeneo hayo shughuli za uzalishaji zitaendelea kama kawaida kwani zoezi hili halita adhiri watu na shughuli zao.
Mafunzo haya ya namna ya kukabiliana na magonjwa ya mlipuko yalianza 2018 kwa washiriki kufundishwa darasani na sasa watafundishwa kwa vitendo zaidi ili waweze kukuza uwelewa wao na jumla ya washiriki ya 65 kutoka katika kila nchi watashiriki.
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa