Mkoa wa Arusha kwa mara ya kwanza umeweza kuadhimisha siku ya ugonjwa wa kupoteza kumbukumbu kwa wazee wenye umri kuanzia miaka 60.
Akitoa taarifa ya maadhimisho hayo yaliambatana na upimaji wa magonjwa mengine kama Kisukari, Presha na Uzito, mwanasaikolojia kutoka hospitali ya Mkoa Mt.Meru bwana Ssenku Shafic Mohamed, amesema zoezi hilo limechukua mda wa wiki nzima.
Na lengo kubwa lilikuwa nikuwapima wazee wenye umri kuanzia miaka 60 na kuendelea ili wajitambue hali yao ya kumbukumbu na magonjwa mengine yasiyoambukiza kama Kisukari,Presha na Uzito.
Aidha, kutokana na zoezi hilo bwana Ssenku amesema wameweza pia kugundua magonjwa mengine kama mtoto wa jicho na tezi dume kwa wazee wanaume.
“Katika hali ambayo hatukitarajia tumeweza kugundua pia ugonjwa wa mtoto wa jicho ambapo kati ya wagonjwa 10 waliokuja hapa watatu kati yao walikuwa wamegundulika na tatizo hilo na pia ugonjwa wa tenzi dume ambapo kati ya wagonjwa 10 wawili wamegundulika na tatizo hilo”.
Amesema wamefanikiwa pia kutoa ushauri wa vyakula sahihi vinavyowafaa wazee na aina ya mazoezi ili kuhakikisha afya zao zinaimarika na wanajikinga na magonjwa mbalimbali hasa la kupoteza kumbukumbu ambalo lina sadikika ni kawaida kwa wazee lakini kitaalamu ni ugonjwa ambao ukipatiwa matibabu mapema hospitali unatibika.
Maadhimisho hayo yanafanyika kila mwaka Septembea 21 duniani na kwa mwaka huu Tanzania kupita mkoa wa Arusha imeadhimisha siku hii kwa mara ya kwanza kwa kushirikiana na nchi nyingine kama vile Mauritius, Nigeria, Zimbabwe, Madasca na Tunisia.
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa