• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
Arusha Regional

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Mkoa
      • Chimbuko/Asili ya eneo
      • Orodha ya wakuu wa Mikoa
    • Dira na dhima
    • Maadili ya msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji Mali
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Maji
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
  • Wilaya
    • Arusha
      • Historia
      • Viongozi
    • Arumeru
      • Historia
      • Viongozi
    • Monduli
      • Historia
      • Viongozi
    • Karatu
      • Historia
      • Viongozi
    • Longido
      • Historia
      • Viongozi
    • Ngorongoro
      • Historia
      • Viongozi
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Arusha
    • Halmashauri ya Arusha
    • Halmashauri ya Meru
    • Halmashauri ya Monduli
    • Halmashauri ya Karatu
    • Halmashauri ya Longido
    • Halmashauri ya Ngorongoro
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Ufugaji
    • Kilimo
    • Viwanda
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Ardhi
    • Utalii
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Picha Mbalimbali
    • Habari
    • Matukio

TBA WAHIMIZWA KUJENGA MAJENGO YA MAKAZI YAKUTOSHA

Posted on: August 4th, 2023


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango amefungua jengo la makazi la kibiashara na kusisitiza kwamba Serikali itaendelea kuziwezesha Taasisi zake kuwa na miradi mikubwa itakayoziwezesha kujitegemea.

Akizungumza katika hafla ya ufunguzi wa jengo la makazi la kibiashara lililo sekei jijini Arusha Dkt. Mpango amesema Serikali imeiruhusu Wakala wa Majengo Nchini (TBA) kushirikiana na sekta binafsi kwa ubia ili kuiwezesha kutekeleza miradi ya kimkakati na itakayoleta tija haraka na hivyo kupunguza utegemezi wake kwa Serikali.

“Nawapongeza kwa ujenzi wa jengo zuri la kisasa, endeleeni na mpango wa kujenga majengo ya aina hii katika maeneo mbalimbali ya kimkakati yatakayowezesha kuhudumia kaya nyingi na zingatieni uhifadhi wa mazingira na kwa kupanda miti na maua na kuweka mifumo mizuri ya kuondosha takataka’ amesema Dkt. Mpango.

Dkt. Mpango ameitaka TBA kufanya uwekezaji wenye tija katika maeneo yake na kuhakikisha wapangaji wa majengo yake wanalipa kodi kwa wakati.

Ameitaka Wizara ya Uwekezaji kuhakikisha inaweka msukumo kwenye ujenzi wa viwanda vya vifaa vya ujenzi ili kupunguza gharama za ujenzi hivyo kuwezesha Serikali kufikia lengo la ujenzi wa nyumba nyingi zitakazokidhi mahitaji ya ongezeko la idadi ya watu.

“Serikali imedhamiria kukuza sekta ya nyumba ili ichangie pato la Taifa na hivyo kukuza uchumi’ amesisitiza Dkt. Mpango.

Kwa upande wake Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa, amesema kuwa azma ya ujenzi huu ni chimbuko la TBA la kutaka kujiendesha  kibiashara na hivyo kupata faida.

“Mfumo wa kisasa wa vitasa janja ili kudhibiti wapangaji wenye madeni na hivyo kusaidia ulipaji wa kodi kwa muda muafaka, lengo la TBA ni kupata mapato zaidi na kujiendesha yenyewe.” amesisitiza Prof. Mbarawa.

Naye Waziri Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Angelina Mabula, ameipongeza TBA kwa kujenga majengo marefu yanayohudumia idadi kubwa ya watu na kusisitiza kuwa majengo hayo yaendane na uwepo na maegesho ya magari.

Amesisitiza kuwa mahitaji ya nyumba nchini zaidi ni 390,981 kwa mwaka wakati nyumba zinazojengwa na taasisi mbalimbali kwa mwaka ni chini ya 2,000.

Amewataka wadau mbalimbali wa ujenzi waendelee kujenga nyumba ili kuendana na ongezeko la idadi ya watu ambapo inakadiriwa takriban watu zaidi ya milioni 1.6 wanaongezeka kila mwaka.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongela amesema jengo hilo lenye sakafu 11 limeongeza thamani ya mji wa Arusha hususani kipindi hiki ambacho idadi ya watalii imeongeza na hivyo kuchochea shughuli za biashara katikati ya jiji.

Awali akitoa taarifa ya mradi huo, Mtendaji Mkuu wa TBA, Arch. Daud Kondoro amesema kukamilika kwa mradi huo utawezesha Wakala kujenga majengo mengine marefu ya makazi na biashara katika eneo la Sekei ili kuhamasisha shughuli za Utalii katika jiji hilo.

“Tumejipanga kuhakikisha miradi ya makazi na biashara iliyoko Canadian – Masaki, jijini Dar es Salaam, Ghana Kotta jijini Mwanza, Tameke Kotta na nyumba 150 (Awamu ya Pili) eneo la Nzunguni  jijini Dodoma inakamilika ili kuiwezesha TBA kuondokana na utegemezi kwa Serikali’ amefafanua Arch. Kondoro.

Jengo la makazi la kibiashara eneo la Sekei lenye sakafu 11 lina uwezo wa kuhudumia kaya 22 na limegharimu zaidi ya shilingi bilioni 6.8 ambapo ujenzi wake umetekelezwa katika awamu nne.




Tangazo

  • TAZAMA MATOKEO YA MTIHANI WA MOCK MKOA DARASA LA SABA 1 July 06, 2023
  • MATOKEO YA MOCK MKOA DARASA LA SABA 2 July 07, 2023
  • TAZAMA MATOKEO YA MOCK MKOA KIDATO CHA NNE July 07, 2023
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • RC MAKONDA ASHUHUDIA UTIAJI SAINI UJENZI WA BARABARA YA ESO - LONGDON NA UKUMBI WA MIKUTANO ARUSHA.

    April 03, 2025
  • RC MAKONDA ATAKA KUPEWA MAJINA YA WATENDAJI WANAOCHOCHEA MIGOGORO YA KIJAMII.

    March 28, 2025
  • KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA NI MAONO NA MAELEKEZO YA RAIS SAMIA- WAZIRI NDUMBARO.

    March 28, 2025
  • OFISI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI YAFANYIA KAZI MALALAMIKO WANANCHI WA MIANZINI ARUSHA.

    March 28, 2025
  • Angalia Zote

Video

UZINDUZI WA BARABARA YA WASO-SALE
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • SALARY SLIP
  • Taarifa ya Mapato
  • Taarifa za Shule (SIS)
  • Takwimu za Sekta ya Elimu (BEMIS)
  • Video

Viunganishi Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Portal ya Watumishi
  • Takwimu
  • TANAPA

Watembeleaji

world map hits counter

Wasiliana Nasi

Mawaliliano mengine

   

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani
    • Maswali ya Mara kwa Mara

Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa