Mfumo wa kutumia teknolojia ya Kompyuta katika kufundishia umeonekana ni mfumo unaorahisisha ufundishaji na kukuza hamasa kwa wanafunzi yakupenda kusoma zaidi.
Shule ya Sekondari Irkisongo iliyopo Wilayani Monduli ni miongoni mwa shule za Mkoa wa Arusha ambazo zimepatiwa Kompyuta 20 kwa ajili ya kufundishia na wanafunzi kujifunza kimtandao.
Kutokana na umuhimu wa teknolojia hiyo katika shule hiyo Katibu Tawala Mkoa wa Arusha Missaile Musa amemuagiza Afisa Tehama Mkoa bwana David Nyangaka kuongeza Komputa nyingine 10 katika shule hiyo.
Bwana Missaile ameyasema hayo alipokuwa akikagua mradi wa Kompyuta katika katika shule hiyo.
Amesema, mfumo wa kufundisha kwa Kompyuta umeonesha kurahisisha ufundishaji kwa walimu na wanafunzi wanajifunza kwa kuona na hivyo kuongeza hamasa yakupenda masomo yao hasa ya sayansi.
Pia, katika ziara yake amefurahishwa na ujenzi wa shule ya Sekondari Meselani ambao utagharimu kiasi cha Milioni 600 hadi kukamilika kwake na kuitaka idara ya elimu katika halmashauri hiyo kuendelea kusimamia vizuri miradi yote.
Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya Monduli Rose Muhina amesema wataendelea kusimamia miradi yote ili iweze kukamilika mapema na wananchi kupata huduma bora.
Katibu Tawala Mkoa amefanya ziara ya kikazi ya siku moja katika Wilaya ya Monduli kwa lengo la kujitambulisha kwa watumishi na kukagua miradi ya maendeleo.
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa