Na Elinipa Lupembe
Imeelewza kuwa, Afya na Usalama Mahali pa kazi, uendane na mabadiliko ya tabia Nchi, ikiwani kauli mbiu ya Maadhimisho ya Siku ya Usalama na Afya Mahali pa kazi mwaka 2024, maadhimisho yaliyofanyika mkoani Arusha, kwenye kiwanja cha General Tyre, eneo la Njiro, Jijini Arusha Aprili, 28, 2024.
Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Usalama na Afya mahala pa kazi (Occupational Safety and Healthy Authority - OSHA), wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Kimataifa ya usalama na afya mahala pa kazi, na kusela kuwa Tanzania inapoadhimisha siku hiyo ni muhimu kuzingatia mabadiliko ya tabia Nchi.
Amesema kuwa, Tanzania inaungana na Dunia nzima na katika kuathimisha siku ya Usalama na Afya Mahala pa kazi, na kusisitiza kuwa, maadhimisho hayo yanaweze kuwa endelevu, kupimika na kutekelezeka yanaenda na kauli mbiu, na kauli mbili ambayo ilitolewa na shirika la kazi Duniani inasema 'athari za mabadiliko ya tabianchi katika usalama na afya.
"Lakini hiyo ni kauli mbiu ya Dunia, na sisi tukaangalia changamoto yetu ni nini linapokuja kuhusu athari za mazingira, kwa hiyo tukasema kama nchi tuje na kauli mbiu yetu ambayo inasema 'athari za mabadiliko ya tabia Nchi katika usalama na afya kazini, sajili eneo lako la kazi katika harakati za kupunguza athari hizo". Amesema Khadija
Wafanyakazi ni nyenzo muhimu sana katika kuleta maendeleo ya Taifa, maendeleo yanayotegemea mazingira ya kazi ambayo ni salama, ambayo shughuli zake za kiuchumi zinatathminiwa, uwezo wake katika kuwalinda wafanyakazi .
Ameongeza kuwa, siku ya leo ina lengo la kukumbushana, kuelimishana, kuhamasishana kuhusu uwepo wa mazingira salama katika maeneo ya kazi ili kulinda nguvu kazi ya Taifa, lakini pia kulinda uwekezaji ambao upo na hatimaye kukuza pato la Taifa na kupata maendeleo tuliyotarajia.
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa