Waziri wa habari, utamaduni,sanaa na michezo Dokta Harrison Mwakyembe amewataka wajasiliamali wa vinyago kutafuta zaidi soko la bidhaa zao za asili ili kukuza kipato na kuendelea kutangaza utalii wa utamaduni.
Ameyasema hayo alipokuwa akuzunguza na wajasilimali wautalii wa utamaduni katika soko la Masai,jiji Arusha.Amesema bidhaa za utalii wa utamaduni ni nembo tosha yakutangaza nchi yetu.
“Ni kweli kuna Changamoto katika ujasiliamali huu wa utalii wa utamaduni hususani kwenye tozo mbalimbali mnazotozwa na mamlaka husua.”
Serikali ipo tayari kwenye mchakato wakutatua Changamoto hii ya tozo na kuona ni namna gani soko la vinyago nchini Tanzania linakuwa na kujulikana zaidi kimataifa, kuliko kwa sasa soko kuu linajulikana lipo jijini Nairobi wakati wazalishaji wakubwa ni watanzania.
Dokta Mwakyembe alikuwa kwenye ziara ya siku 3 Mkoani Arusha,ambapo ameweza kufungua redio mpya ya kijamii (TBC FM),aliweza kutembelea kituo cha redio cha Sunrise,alifungua mkutano wa maafisa habari na mawasilino serikali,ameweza kukutana na wadau wa utamaduni,sanaa na michezo na ameweza kutembelea soko la vinyago la jijini Arusha.
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa