VIJANA KARATU WAISHUKURU SERIKALI YA MAMA SAMIA KWA MIKOPO ISIYO NA RIBA; YAWAWEZESHA KUANZISHA KIWANDA CHA KUOKA VITAFUNWA.
Na Elinipa Lupembe
Vijana wa Kikundi cha Amani Barazani Youth Group cha wilaya ya Karatu, wameishukuru serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwathamini vijana wakitanzani na kuwatengenezea fursa za kujiinua Kiuchumi zinazowaweesha kujiajiri na kuajiri vijana wengine.
Mwenyekiti wa kikundi hicho, James Emmanuel amesema kuwa kukundi kina wanachama 10 na kilianza mradi wa kupika maandazi kwa mtaji kwa kuchangishana fedha kupitia kikundi chao cha kuweka na kukopa na baadaye kuwezeshwa na ofisi ya mkurugenzi halmashauri ya Karatu kwa kupata mkopo usiokuwa na riba wa shilingi milioni 8 kwa awamu mbili.
Fedha hizo ziliwawezesha kukuza mtani na kununua jiko kubwa la kuokea vitafunwa na kuanza kuoka mikate na keki, biashara ambayo inaendelea kukua na kushamiri wakiwa wameliteka soko la vitafunwa wilaya ya Karatu na vitongoji vyake.
Mwenyekiti huyo ameweka wazi kuwa awali waliposikia habari za mikopo hawakuamini, wakidhani ni mambo ya siasa, lakini baada ya kukutana na watalamu na kuwapa elimu ya mikopo na ujasiriamali, taratibu zote na hatimaye kupata mkopo, ndipo walipoamini Serikali ya mama Samia iko makini na ina mikakati imara kuhusu vijana.
"Kupitia biashara hii, licha ya kutuinua kiuchumi imetuwezesha kujiari na kuajiri vijana wengine 13, vijana 6 wakiwa na ajira rasmi na vijana 7 vibarua kazi za muda, zaidi imetuwezesha kukutana na wadau wengi wanaondelea kutupa uzoefu wa kukua katika masoko na kukuza biashara yetu"Amesema Emmanuel.
Aidha amewasihi vijana wengie kutumia fusra hiyo adhimu kwa kuwa kunao utofauti mkubwa kati ya mikopo inayotolewa na serikali na ile ya benki yenye riba kubwa hasa ukizingatia vijana wengi hawana vigezo vya kuweza kukopeshwa na benki, sheria zao zinamuhitaji mkopaji kumiliki mali zisizohamishika ambazo kimsingi vijana hawana.
Ameongeza kuwa licha ya kuwa soko la vitafunwa linaushindani mkunwa lakini kutokana na ubora wa bidhaa zao zimeweza kupenya sokoni na kupokelewa kwa mwitikio mkubwa unaowafanya kutamani kumiliki kiwanda kikubwa kitakachozalisha bidhaa nyingi zitakazopatikana Karatu na vitongoji vyake na hatimaye maneneo mengine nje ya Karatu na ikiwezekana mkoa wa Arusha na Tanzania nzima.
Hata hivyo wameishukuru Ofisi ya mkuu wa mkoa wa Arusha, kwa uongozi wa Mhe. John V.K. Mongella kwa fursa nyingi anazozitoa kwa vijana kwa kuwakutanisha na watalamu, wadau na wateja pinda yanapotokea maonesho makubwa yanayohusu vijana na biashara, fursa ambazo zinawawezesha kubadilishana uzoefu, kutambua fursa zaidi pamoja na kukua kibiashara.
#ArushaFursaLukuki
#KaziInaendelea
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa