• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
Arusha Regional

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Mkoa
      • Chimbuko/Asili ya eneo
      • Orodha ya wakuu wa Mikoa
    • Dira na dhima
    • Maadili ya msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji Mali
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Maji
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
  • Wilaya
    • Arusha
      • Historia
      • Viongozi
    • Arumeru
      • Historia
      • Viongozi
    • Monduli
      • Historia
      • Viongozi
    • Karatu
      • Historia
      • Viongozi
    • Longido
      • Historia
      • Viongozi
    • Ngorongoro
      • Historia
      • Viongozi
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Arusha
    • Halmashauri ya Arusha
    • Halmashauri ya Meru
    • Halmashauri ya Monduli
    • Halmashauri ya Karatu
    • Halmashauri ya Longido
    • Halmashauri ya Ngorongoro
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Ufugaji
    • Kilimo
    • Viwanda
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Ardhi
    • Utalii
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Picha Mbalimbali
    • Habari
    • Matukio

VIJANA WA SKAUTI WAENDELEA  KUHASISHA JAMII JUU YA UTUNZAJI WA MAZINGIRA NA VYANZO VYA MAJI......

Posted on: October 9th, 2023

Na Elinipa Lupembe


Vijana 23 wa Skauti waliojitolea kutembea na kuhamasisha utunzaji wa mazingira na vyanzo vya maji nchini, kwa kufanya matembezi ya hiari kuelekea kilele cha wiki ya vijana na kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru 2023 mkoani Manyara, wametakiwa kuhamasisha jamii bila kuchoka suala zima la utunzaji wa mazingira.


Rai hiyo imetolewa na mkuu wa wilaya ya Arusha, Mhe. Felician Mtahengerwa, kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Arusha wakati wa kuwapokea vijana hao 23 wa skauti wakitokea mkoa  wa kilimanjaro kupanda mlima Kilinjaro wakielekea mkoani Manyara kwenye kilele cha mbio za Mwenye wa Uhuru 2023.


Mhe. Mtahengerwa, licha ya kuwapongeza vijana hao kwa uzalendo wa kujitoa kuhamasisha jamii katika utunzaji wa mazingira na vyanzo vya maji, amewata kuhamasisha jamii husuani vijana wenzao kuhakikisha wanajikita katika utunzaji wa mazingira kwa kuwa ndio rasilimali kuu kwa binadamu na viumbe wote.


"Niwapongeze kwa uzalendo mlioonesha lakini pia mnapaswa kutambua vijana mnalo jukumu kubwa la kulitumikia Taifa kwa kuhamasisha jamii umuhimu na faida za utunzaji wa mazingira, kwa kutambua kuwa mazingira ni uhai wa viumbe vyote ikiwemo wanadamu" Amesema Mhe. Mtahengera


Hata hivyo vijana hao wameishukuru serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwapa vijana fursa na vipaumbele vingi kushiriki katika ujenzi wa taifa pamoja na kushiriki kwenye shughuli mbalimblai za kijamii na za maendeleo nchini.


Mratibu Mkuu wa Zoezi la Kizalendo, Kamishna wa Skaut wilaya ya Bariadi, Mayunga Kidoyayi amesema kuwa lengo la matembezi hayo ya hiari ni kuendelea kuikumbusha jamii jumbe  za Mwenge wa Uhuru 2023 uliobeba kauli mbiu Tunza Mazingira, okoa vyanzo vya maji kwa Ustawi wa viumbe hai kwa uchumi wa Taifa.


Amesema kuwa Mwenge wa Uhuru 2023 umepita mikoa yote ya Tanzania ukiwa na jumbe mbalimbali lakini vijana hao wanapita kuikumbusha  na kuhamasiha jamii kuzingatia jumbe hizo ikiwemo mapambano dhidi ya rushwa, kujinga na magonjwa ya UKIMWI na Malaria, umuhimu wa lishe bora, kupiga vita matumizi ya Madawa ya Kulevya pamoja na utunzaji wa mazingira kwa maendelo ya jamii na uchumi wa Taifa.

Kiongozi wa Kikosi Maalum cha Skaut, Omary Ahmed Kasaka, amesema kuwa wao kama vijana wamepita kuelekea mlima Kilimanjaoro na kuielemisha jamii umuhimu wa kutunza mazingira hususani wananchi waishio pembezoni mwa mlima Kilimanjaro, ambao mara nyingi kunatokea moto unaosababishwa na shughuli za kibainadamu.


"Sisi kama vijana wa kitanzania, tunaridhishwa na kazi kubwa inayofanywa na Mhe. Rais hivyo tuko tayari kujitoa kuunga mkono juhudi zote  za serikali, tunakwenda Manyara kwa kutembea kwa mguu Km 162, kushiriki kilele cha wiki ya Vijana, kumbukumbu ya Mwl. Jk Nyerere pamoja na kiele cha Mbio za mwenge wa Uhuru 2023" Amesema Omary Ahmed Kasaka


#ARUSHA FURSA LUKUKI

#KaziInaendelea


Tangazo

  • TAZAMA MATOKEO YA MTIHANI WA MOCK MKOA DARASA LA SABA 1 July 06, 2023
  • MATOKEO YA MOCK MKOA DARASA LA SABA 2 July 07, 2023
  • TAZAMA MATOKEO YA MOCK MKOA KIDATO CHA NNE July 07, 2023
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • RC MAKONDA ASHUHUDIA UTIAJI SAINI UJENZI WA BARABARA YA ESO - LONGDON NA UKUMBI WA MIKUTANO ARUSHA.

    April 03, 2025
  • RC MAKONDA ATAKA KUPEWA MAJINA YA WATENDAJI WANAOCHOCHEA MIGOGORO YA KIJAMII.

    March 28, 2025
  • KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA NI MAONO NA MAELEKEZO YA RAIS SAMIA- WAZIRI NDUMBARO.

    March 28, 2025
  • OFISI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI YAFANYIA KAZI MALALAMIKO WANANCHI WA MIANZINI ARUSHA.

    March 28, 2025
  • Angalia Zote

Video

UZINDUZI WA BARABARA YA WASO-SALE
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • SALARY SLIP
  • Taarifa ya Mapato
  • Taarifa za Shule (SIS)
  • Takwimu za Sekta ya Elimu (BEMIS)
  • Video

Viunganishi Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Portal ya Watumishi
  • Takwimu
  • TANAPA

Watembeleaji

world map hits counter

Wasiliana Nasi

Mawaliliano mengine

   

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani
    • Maswali ya Mara kwa Mara

Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa