• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
Arusha Regional

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Mkoa
      • Chimbuko/Asili ya eneo
      • Orodha ya wakuu wa Mikoa
    • Dira na dhima
    • Maadili ya msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji Mali
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Maji
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
  • Wilaya
    • Arusha
      • Historia
      • Viongozi
    • Arumeru
      • Historia
      • Viongozi
    • Monduli
      • Historia
      • Viongozi
    • Karatu
      • Historia
      • Viongozi
    • Longido
      • Historia
      • Viongozi
    • Ngorongoro
      • Historia
      • Viongozi
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Arusha
    • Halmashauri ya Arusha
    • Halmashauri ya Meru
    • Halmashauri ya Monduli
    • Halmashauri ya Karatu
    • Halmashauri ya Longido
    • Halmashauri ya Ngorongoro
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Ufugaji
    • Kilimo
    • Viwanda
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Ardhi
    • Utalii
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Picha Mbalimbali
    • Habari
    • Matukio

WAFAMASIA NA WAMILIKI MADUKA YA DAWA; WAONYWA KUTOA  DAWA WA MGONJWA ASIYEKUWA NA CHETI CHA DAKTARI..

Posted on: November 17th, 2023

Na Prisca Libago


Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu ametoa onyo kali kwa wafamasi na wamiliki wa maduka ya dawa waotoa dawa kwa mgonjwa asiyekuwa na cheti cha daktari, kufanya hivyo ni kuendeleza tatizo la usugu wa vimelea vya magonjwa dhidi ya dawa na kuhatarisha afya za watu.


Waziri Ummy amesema hayo Novemba 17, 2023, wakati akifunga Kongamano la Tatu, la Usugu wa Vimelea dhidi ya Dawa na kufungua rasmi wiki ya uhamasishaji na uelimishaji jamii juu ya matumizi sahihi ya dawa inayoanza Novemba 18 hadi 24, 2023.


“Nataka wafamasia wote nchini kuacha mara moja tabia ya kutoa dawa, ikiwemo za Antibiotiki bila cheti cha daktari na tukimkamata yeyote atakayekaidi atapigwa faini kubwa kama sio kumfungia duka kabisa.” Amesema Waziri Ummy.


Amesema, kutakuwa na timu maalum ya kufanya kaguzi za kushtukiza, kwenye maduka ya dawa, na kusisitiza mfamasia atakaebainika kutoa dawa za Antibiotiki bila cheti cha daktari, atapigwa faini na kufikishwa mahakamani ili sheria ichukue mkondo wake.


Aidha, Waziri Ummy amewataka wataalamu wa Afya, kuzingatia Mwongozo wa Taifa wa Matibabu wanapo wahudumia wagonjwa ili kufanikisha kampeni ya ‘Afya Moja’ yenye lengo la mapambano ya Usugu wa Vimelea vya Magonjwa dhidi ya Dawa.


“Naendelea kusisitiza kwa wataalam wetu wa Afya, hakikisheni mnazingatia Mwongozo wa Taifa wa Matibabu, nawaomba sana hasa katika kuwaandikia wagonjwa dawa, maana tumepata kesi tunaona mtu ana UTI anaandikiwa Antibiotic mpaka saba.” Amesema Waziri Ummy


Amesema, iwapo watoa huduma za Afya watafuata Mwongozo wa Taifa wa Matibabu itawezesha Serikali kwenda kwa kasi katika mapambano ya Usugu wa vimelea dhidi ya dawa.


Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Tumaini Nagu amewaasa wataalam wa kilimo, uvuvi, mifugo na afya kuzingatia dhana ya mwaka huu ya Kongamano hilo kwa kuendelea kuboresha njia za mapambano ya tatizo la usugu wa vimelea dhidi ya dawa na kutoa elimu ya uwelewa kwa jamii ili kufikia lengo la mpango huo.


Tangazo

  • TAZAMA MATOKEO YA MTIHANI WA MOCK MKOA DARASA LA SABA 1 July 06, 2023
  • MATOKEO YA MOCK MKOA DARASA LA SABA 2 July 07, 2023
  • TAZAMA MATOKEO YA MOCK MKOA KIDATO CHA NNE July 07, 2023
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • RC MAKONDA ASHUHUDIA UTIAJI SAINI UJENZI WA BARABARA YA ESO - LONGDON NA UKUMBI WA MIKUTANO ARUSHA.

    April 03, 2025
  • RC MAKONDA ATAKA KUPEWA MAJINA YA WATENDAJI WANAOCHOCHEA MIGOGORO YA KIJAMII.

    March 28, 2025
  • KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA NI MAONO NA MAELEKEZO YA RAIS SAMIA- WAZIRI NDUMBARO.

    March 28, 2025
  • OFISI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI YAFANYIA KAZI MALALAMIKO WANANCHI WA MIANZINI ARUSHA.

    March 28, 2025
  • Angalia Zote

Video

UZINDUZI WA BARABARA YA WASO-SALE
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • SALARY SLIP
  • Taarifa ya Mapato
  • Taarifa za Shule (SIS)
  • Takwimu za Sekta ya Elimu (BEMIS)
  • Video

Viunganishi Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Portal ya Watumishi
  • Takwimu
  • TANAPA

Watembeleaji

world map hits counter

Wasiliana Nasi

Mawaliliano mengine

   

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani
    • Maswali ya Mara kwa Mara

Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa