Mkuu wa Mkoa wa Arusha mheshimiwa Idd Kimanta, amemtaka Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Karatu bwana Waziri Mourice, kuhakikisha ujenzi wa soko la Karatu unakamirika ifikapo mwishoni mwa mwezi huu wa tisa.
Ameyasema hayo alipokuwa akikagua ujenzi wa soko la Karatu linalotarajia kuchukua wafanyabiashara takribani 198.
Kimanta amesema, soko hilo linatakiwa kuisha kabla msimu wa mvua haujaanza ili wafanyabiashara hao wapate mazingira mazuri ya kufanyia biashara zao.
Soko hilo linauwezo wa kuchukua wafanyabiashara 202 na lenye hadhi nzuri ya kutoa nafasi ya kufanyia biashara kwa uhuru zaidi.
Mkuu wa Mkoa amekagua ujenzi wa soko hilo, ikiwa na moja ya shughuli anazozifanya katika ziara yake ya kikazi ya kukagua miradi ya maendeleo katika wilaya hiyo.
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa