• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
Arusha Regional

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Mkoa
      • Chimbuko/Asili ya eneo
      • Orodha ya wakuu wa Mikoa
    • Dira na dhima
    • Maadili ya msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji Mali
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Maji
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
  • Wilaya
    • Arusha
      • Historia
      • Viongozi
    • Arumeru
      • Historia
      • Viongozi
    • Monduli
      • Historia
      • Viongozi
    • Karatu
      • Historia
      • Viongozi
    • Longido
      • Historia
      • Viongozi
    • Ngorongoro
      • Historia
      • Viongozi
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Arusha
    • Halmashauri ya Arusha
    • Halmashauri ya Meru
    • Halmashauri ya Monduli
    • Halmashauri ya Karatu
    • Halmashauri ya Longido
    • Halmashauri ya Ngorongoro
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Ufugaji
    • Kilimo
    • Viwanda
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Ardhi
    • Utalii
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Picha Mbalimbali
    • Habari
    • Matukio

WAKULIMA ARUSHA WAVUTIWA NA MAHINDI YENYE PROTINI NA MAHARAGE LISHE

Posted on: July 13th, 2024


Wakulima wa Mkoa wa Arusha wamekiri kuvutiwa na elimu kuhusu mahindi na maharage lishe yaliyofanyiwa utafiti katika Kituo cha Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) kituo cha Selian, kwa kuwa yatakwenda kujibu changamoto ya utapiamlo na mavuno hafifu kutokana na mabadiliko ya tabia nchi.


Wakulima hao wamekiri hayo mapema leo wakati wa maadhimisho ya Kilimo biashara yaliyofanyika kwa muda wa siku mbili katika viwanja vya TARI Seliani ambapo wamesema wengi hawakuwa wakifahamu kuhusu mahindi yenye lishe ya protini.


Loveness Urio mkulima kutoka Maji ya chai amesema “tumefurahi kupata elimu hii mimi sikuwahi kusikia kuhusu mahindi lishe yenye protini sasa tunaomba elimu hii iletwe hadi vijijini ili wakulima wazalishe mahindi hayo pamoja na maharage lishe, tunataka tuyalime watoto wetu wasipate utapiamlo”.


Naye Tajiri Laizer mkulima kutoka kata ya Lemanyata  ameongeza kuwa , “tunashukuru kupata elimu ya kilimo bora katika maonyesho haya, tumejifunza kuhusu mahindi na maharage lishe kwetu vyakula vinavyotumika huenda sio lishe kamili hivyo tunaoma elimu hii nasi tuweze kulima vyakula ambavyo vitatupa kinga mwilini na kuimarisha afya zetu”.


Kwa upande wake Elieshi kitomari mkulima kutoka Maji ya chai amesema kupitia maonyesho hayo ameweza kujifunza kuhusu matumizi sahihi ya mbolea pamoja na kilimo bora cha mbogamboga 


Mtafiti kutoka TARI Selian,Moses Bayinga ameeleza kuwa, wakulima 450 wameshiriki maonyesho ya kilimo biashara kwa mwaka 2024 yaliyofanyika Julai 12 na 13 na wamefikiwa  na teknolojia mbalimbali kutoka kampuni  na taasisi 14 ambazo zinahusika na pembejeo za kilimo lengo likiwa ni kuwahimiza wakulima kutumia teknolijia bunifu za kilimo kwa ajili ya uhakika wa chakula na lishe.


Akizungumza kwa niaba ya Katibu Tawala Mkoa wa Arusha, Afisa Kilimo Mkoa, Danieli Loiruk ametoa wito kwa wakulima kuacha kilimo cha mazoea bali wazingatie lishe na mahitaji ya soko.


Amesema wakulima wanapaswa kuwa na mtazamo wa ujasiriamali watumie teknolojia zinazo zalishwa TARI ili zijibu tatizo la mabadiliko ya tabia nchi na lishe pamoja na kupata ushauri kutoka kwa maafisa kilimo.


Tangazo

  • TAZAMA MATOKEO YA MTIHANI WA MOCK MKOA DARASA LA SABA 1 July 06, 2023
  • MATOKEO YA MOCK MKOA DARASA LA SABA 2 July 07, 2023
  • TAZAMA MATOKEO YA MOCK MKOA KIDATO CHA NNE July 07, 2023
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • RC MAKONDA ASHUHUDIA UTIAJI SAINI UJENZI WA BARABARA YA ESO - LONGDON NA UKUMBI WA MIKUTANO ARUSHA.

    April 03, 2025
  • RC MAKONDA ATAKA KUPEWA MAJINA YA WATENDAJI WANAOCHOCHEA MIGOGORO YA KIJAMII.

    March 28, 2025
  • KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA NI MAONO NA MAELEKEZO YA RAIS SAMIA- WAZIRI NDUMBARO.

    March 28, 2025
  • OFISI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI YAFANYIA KAZI MALALAMIKO WANANCHI WA MIANZINI ARUSHA.

    March 28, 2025
  • Angalia Zote

Video

UZINDUZI WA BARABARA YA WASO-SALE
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • SALARY SLIP
  • Taarifa ya Mapato
  • Taarifa za Shule (SIS)
  • Takwimu za Sekta ya Elimu (BEMIS)
  • Video

Viunganishi Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Portal ya Watumishi
  • Takwimu
  • TANAPA

Watembeleaji

world map hits counter

Wasiliana Nasi

Mawaliliano mengine

   

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani
    • Maswali ya Mara kwa Mara

Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa