• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
Arusha Regional

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Mkoa
      • Chimbuko/Asili ya eneo
      • Orodha ya wakuu wa Mikoa
    • Dira na dhima
    • Maadili ya msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji Mali
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Maji
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
  • Wilaya
    • Arusha
      • Historia
      • Viongozi
    • Arumeru
      • Historia
      • Viongozi
    • Monduli
      • Historia
      • Viongozi
    • Karatu
      • Historia
      • Viongozi
    • Longido
      • Historia
      • Viongozi
    • Ngorongoro
      • Historia
      • Viongozi
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Arusha
    • Halmashauri ya Arusha
    • Halmashauri ya Meru
    • Halmashauri ya Monduli
    • Halmashauri ya Karatu
    • Halmashauri ya Longido
    • Halmashauri ya Ngorongoro
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Ufugaji
    • Kilimo
    • Viwanda
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Ardhi
    • Utalii
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Picha Mbalimbali
    • Habari
    • Matukio

WAKUU WA IDARA ZA UTAWALA NA RASILIMALI WATU NCHINI WATAKIWA KUSIMAMIA MAJUKUMU YAO KWA MUJIBU WA SHERIA.....

Posted on: October 11th, 2023

Na Elinipa Lupembe


Wakuu wa Idara za Utawala na  Rasilimaliwatu wametakiwa kusimamia majukumu yao kwa mujibu wa sheria kwa kuzingatia viapo vya Utumishi wa Umma walivyoapa kusimamia na kuwahudumia watumishi wa Umma kwa kuzingatia Kanuni sheria na taratibu za utumishi.


Rai hiyo imetolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. George Simbachawene, wakati akifungua mkutano wa mwaka wa viongozi hao uliofanyika kwenye ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa Arusha (AICC) mkoani Arusha.


Mhe. Simbachawene ameweka wazi kuwa kutokana na utafiti uliofanywa na Wizara yake mwaka 2022, umebaini kuna maeneo Maafisa Raslimaliwatu hawatekelezi majukumu yao kulingana na viapo vyao ambavyo vinawawezesha kuwa na Utumishi uliotukuka ili kufikia malengo ya taasisi zao na serikali kwa ujumla.


Amesisitiza kufanyia kazi matokeo ya tafiti hiyo kwa maafisa hao kufanya kazi kwa weledi kwa kuzingatia sheria, kanuni, taratibu na miongozo, chukueni hatua katika kuboresha utawala na usimamizi wa rasilimali watu katika maeneo yenu.


Hata hivyo amekemea tabia ya baadhi ya Maafisa Tawala  matumizi mabaya ya madaraka ikiwemo upendeleo, matumizi binafsi Katika Utumishi jambi ambalo limedidimiza na kukwamisha taasisi  kufikia malengo na kuwataka maafisa hao  kujitathimini na kiwacha tabia hizo.


"Kuna maeneo ya ambayo Maafisa Rasilimaliwatu wanalegalega katika kusimamia Sera,kanuni, sheria, maadili na miongozo,huo sio utendaji unaoridhisha kwa kuwa kuna watumishi wengi hawawajibiki  ipasavyo na kutahadharisha kwamba eneo litakalobainika  lina mapungufu, Serikali haitasitaa kuwachukulia hatua hivyo kabla hawakachukukuwa hatua wakatekeleze majukumu yao ipasavyo.


Ameongeza kuwa ofisi yake imekuwa ikipokea  malalamiko ya watumishi Wastaafu hivyo akawataka maafisarasilimali watu wawe wanakaa na watumishi wanaokaribia kustaafu Ili kuwapatia elimu  wawaandae vizuri,wawasilishe michango yao mapema Ili wanapostaafu wasisumbike ,wasiteseke na hatimae kufariki mapema wakihangaika mafao yao.


Naye Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Xavier Daudi, amebainisha kwa, lengo la kikao kazi hicho kukumbushana utekelezaji wa majukumu yao, kujadili changamoto zinazokwamisha utekelezaji na namna ya kuzitatua, kupeana maelekezo pamoja na kubadilishana uzoefu katika utekelezaji wa majukumu ya kazi kwa kuzingatia shabaha na vipaumbele vya kiataifa.


Aidha amewapongeza watendaji hao kwa kazi kubwa wanayoifanya watalamu hao, kwa utekelezaji wa majukumu yenu ya siku hasi siku, ninawapongeza watendaji wa ofisi yangu, ndio yenye dhamana Rasilimali kiongozi katika raismali nyingi nchini ni fusa sahihi ya kupeana maelekezipo na kujadiliana juu ya ustawi wa sekata hii muhimu ya maendeleo ya nchi yetu, uongozi wa mkoa wa Arusha kwa mapokezi.


Hata hivyo mkuu wa mkoa Arusha Mhe. John Mongela licha ya kuwakaribisha kwenye mkoa wa Arusha,

Maafisa Tawala kufurahia mandhari na hali ya hewa  nzuri ambayo watu kutoka mataifa mbalimbali hufika mkoani Arusha na kufurahia.


Aidha amewahimiza watalamu hao, kuhakikisha wanapata wasaa wa kufanya utalii wa ndani kwa kutembelea vivutio vya Utalii ndani ya mkoa wa Arusha ili  kumuunga mkono Rais Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassani kwa kampeni yanu ya kimataifa ya Royal Tour.


Kikao kazi hicho  cha Wakuu wa Idara za Utawala na rasilimali watu  Katika Utumishi wa umma kimeandaliwa na ofisi ya Rais,manegmenti ya Utumishi wa umma na utawala bora kauli mbiu yake inasema Usimamizi wa raslimali  watu unaozingatia maadili,Sheria na uwajibikaji  na matumizi ya tehama  ni msingi wa huduma bora Katika Utumishi  wa umma.


#arushafursalukuki

#kaziinaendelea






Tangazo

  • TAZAMA MATOKEO YA MTIHANI WA MOCK MKOA DARASA LA SABA 1 July 06, 2023
  • MATOKEO YA MOCK MKOA DARASA LA SABA 2 July 07, 2023
  • TAZAMA MATOKEO YA MOCK MKOA KIDATO CHA NNE July 07, 2023
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • RC MAKONDA ASHUHUDIA UTIAJI SAINI UJENZI WA BARABARA YA ESO - LONGDON NA UKUMBI WA MIKUTANO ARUSHA.

    April 03, 2025
  • RC MAKONDA ATAKA KUPEWA MAJINA YA WATENDAJI WANAOCHOCHEA MIGOGORO YA KIJAMII.

    March 28, 2025
  • KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA NI MAONO NA MAELEKEZO YA RAIS SAMIA- WAZIRI NDUMBARO.

    March 28, 2025
  • OFISI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI YAFANYIA KAZI MALALAMIKO WANANCHI WA MIANZINI ARUSHA.

    March 28, 2025
  • Angalia Zote

Video

UZINDUZI WA BARABARA YA WASO-SALE
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • SALARY SLIP
  • Taarifa ya Mapato
  • Taarifa za Shule (SIS)
  • Takwimu za Sekta ya Elimu (BEMIS)
  • Video

Viunganishi Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Portal ya Watumishi
  • Takwimu
  • TANAPA

Watembeleaji

world map hits counter

Wasiliana Nasi

Mawaliliano mengine

   

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani
    • Maswali ya Mara kwa Mara

Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa