• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
Arusha Regional

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Mkoa
      • Chimbuko/Asili ya eneo
      • Orodha ya wakuu wa Mikoa
    • Dira na dhima
    • Maadili ya msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji Mali
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Maji
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
  • Wilaya
    • Arusha
      • Historia
      • Viongozi
    • Arumeru
      • Historia
      • Viongozi
    • Monduli
      • Historia
      • Viongozi
    • Karatu
      • Historia
      • Viongozi
    • Longido
      • Historia
      • Viongozi
    • Ngorongoro
      • Historia
      • Viongozi
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Arusha
    • Halmashauri ya Arusha
    • Halmashauri ya Meru
    • Halmashauri ya Monduli
    • Halmashauri ya Karatu
    • Halmashauri ya Longido
    • Halmashauri ya Ngorongoro
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Ufugaji
    • Kilimo
    • Viwanda
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Ardhi
    • Utalii
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Picha Mbalimbali
    • Habari
    • Matukio

WANAWAKE SALE WAMSHUKURU RAIS Dkt. SAMIA SULUHU HASSAN KWA UPANUZI WA KITUO CHA AFYA...

Posted on: November 15th, 2023

Na Elinipa Lupembe


Kata ya Sale, iko umbali wa takribani Kilomita 49  kutoka makao makuu ya wilaya ya Ngorongoro yaliyoko eneo la Waso kata ambayo ina wakazi 6,579, wanaojishughulisha na kilimo na ufugaji.


Kwa kipindi kirefu, hawakuwahi kuwa na kituo cha afya, zaidi walikuwa na zahanati ndogo ya kijiji, ambayo ilitoa huduma ambazo, kutokana na ongezeko la idadi ya watu, ilifikia kuelemewa na kushindwa  kutoa hudmua stahiki kwa wote.


Wananchi wa Sale hususani wanawake, walilazimika kwenda eneo la Waso, kupata huduma za kujifungua jambo ambalo liliwagharimu muda na fedha na kusababisha vifo vya kina mama na watoto wakati wa kujifungua, kutokana na ucheleweshwaji wa upatikanaji wa huduma.


Jenifa Ismael Legina, licha ya kuishukuru Serikali ya awamu ya sita kwa kujenga kituo cha afya Sale, amethibitisha, kituo hicho kitaondoa vifo visivyo vya lazima, hasa kwa wanawake wakati wa kujifungua kwa kuwa, kinatoa huduma bora huku kikiwa na madaktari wazuri wenye moyo wa kuwahudumia.


 "Kuna wajawazito walipoteza maisha kwa kukosa huduma ya kuongezewa damu, ilikuwa mpaka uenda Waso, kama huna pesa, ilikuwa ni tatizo kwa familia nyingi, wakati mwingine tulilazimika kuchangishana ili mtu akapate huduma, kwa sasa hakuna tena hayo maisha" Ameweka wazi Jenifa.


Naye Bi. Hosiana, mama wa watoto watatu ambaye ni mgonjwa wa kwanza kujifunga katika wodi ya wazazi, amesema , watoto wake wawili alilazimika kufunga safari mpaka  Waso, umbali wa zaidi ya Km 49 kutoka eneo hilo,  ili kwenda kujifungua jambo ambalo liliwapa gharama kubwa za fedha na muda, lakini wapo kinamama waliopoteza maisha kwa kuchelewa kupata huduma za kujifungua.


"Ninamshukuru mama Samia, nimekuwa wa kwanza kulazwa kwenye wodi moya ya wazazi, ninamuombe aendelee kutuongoza watanzania, matunda  yake tunayaona hadi huku vijijini"Amesema Hosiana.


Serikali ilitoa shilingi milioni 500 kwa ajili ya upanuzi wa zahanati ya Sale ili kuwa na hadhi ya kituo cha afya, na tayari kituo kimeanza kutoa huduma kwa jamii.


#TupoKazini

#tutakufikiapopoteulipo

#ArushaFursaLukuki

Tangazo

  • TAZAMA MATOKEO YA MTIHANI WA MOCK MKOA DARASA LA SABA 1 July 06, 2023
  • MATOKEO YA MOCK MKOA DARASA LA SABA 2 July 07, 2023
  • TAZAMA MATOKEO YA MOCK MKOA KIDATO CHA NNE July 07, 2023
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • RC MAKONDA ASHUHUDIA UTIAJI SAINI UJENZI WA BARABARA YA ESO - LONGDON NA UKUMBI WA MIKUTANO ARUSHA.

    April 03, 2025
  • RC MAKONDA ATAKA KUPEWA MAJINA YA WATENDAJI WANAOCHOCHEA MIGOGORO YA KIJAMII.

    March 28, 2025
  • KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA NI MAONO NA MAELEKEZO YA RAIS SAMIA- WAZIRI NDUMBARO.

    March 28, 2025
  • OFISI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI YAFANYIA KAZI MALALAMIKO WANANCHI WA MIANZINI ARUSHA.

    March 28, 2025
  • Angalia Zote

Video

UZINDUZI WA BARABARA YA WASO-SALE
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • SALARY SLIP
  • Taarifa ya Mapato
  • Taarifa za Shule (SIS)
  • Takwimu za Sekta ya Elimu (BEMIS)
  • Video

Viunganishi Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Portal ya Watumishi
  • Takwimu
  • TANAPA

Watembeleaji

world map hits counter

Wasiliana Nasi

Mawaliliano mengine

   

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani
    • Maswali ya Mara kwa Mara

Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa