Na Elinipa Lupembe
Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mhe. Paul Christian Makonda amewataka watumishi wa Umma mkoa wa Arusha kuwahurumia wananchi kwa kutatua changamoto zao bila kujali hali zao na sio kuwa chanzo cha migogoro baina yao.
Mhe. Makonda ameendelea kusisitiza hayo, kwenye Mkutano wa Hadhara na wananchi wa Halmashauri ya Arusha, Wilaya ya Arumeru, kwenye kiwanja cha Kanisa Katoliki Ngaramtoni Mei 28, 2024.
Ametumia mkutano huo kusikiliza kero za wanannchi na kuzitafutia ufumbuzi ikiwemo migogoro ya ardhi, rushwa, dhuruma, ubadhilifu na uzembe kwa baadhi ya watumishi wa Umma.
Aidha, amewataka wananchi kuendelea kuiamini Serikali ya awamu ya sita chini ya jemadari Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa anayoifanya ya kuwahudumia wananchi kwa kutoa fedha nyingi zinazotekelza miradi ya maendeleo katika sekta zote miradi ambayo kwa asilimia kubwa imesogeza hudumq karibu na wananchi.
"Tuendelee kumuamini Mama Samia, kwa kazi kubwa anayoifa ya kuwahudumia wananchi, na kuendelea kumuunga mkono, sisi wasaidizi wake tutaendelea kupambania haki zenu, msiogope". Amesisitiza Mhe. Makonda.
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa