Na Elinipa Lupembe.
Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Hamidu Aweso (MB) amefika Wilaya ya Monduli kwa lengo la kunusuru Bwawa la Nanja, baada ya kingo za Bwawa hilo kumeguka kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha, bwawa ambalo ni chanzo pekee cha Maji, kiachotegemewa na wafugaji wa vijiji 30 katika
Akizungumza na mamia wa wananchi wa Kata za Lepruko, Sepeko, na Makuyuni, Mhe. Aweso ametoa maelekezo kwa Wataalamu wa Wizara ya maji kutumia taaluma zao kuhakikisha Bwawa, linakarabatiwa kwa dharura na kwa haraka, ili kudhibiti maji kuendelea kupotea wakati wakisubiri kufanya usanifu wa kina nyakati za kiangazi, bwawa hilo liweze kukarabatiwa kwa uhakika zaidi
Mhe. Aweso amesisitiza kuwa, pamoja na ugumu wa kukarabati bwawa hilo wakati likiwa na maji, amewaagiza wataalamu wa Wizara ya Maji, kufanya maamuzi magumu ili kufanikisha kulinusuru Bwawa hiko, kwani hakuna namna nyingine.
Naye Mbunge wa Jimbo la Monduli Mhe. Fred Edward Lowassa amesema kuwa, Bwawa hilo ni tegemeo kubwa la wanachi wa Monduli, ikiwa ni chanzo cha maji kinachotegemewa kwa matumizi ya Binadamu, mifugo na wanyamapori na kuiomba Serikali kupitia Wizara yenye dhamana kuona namna ya kufanua ukarabati kwa dharura ili kuondoa adha inayowakabili wananchi hao.
Aidha, Wakizungumza katika nyakati tofauti madiwani wa kata zinazoguswa na bwawa hilo wameishukuru Serikali inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuwafikia kwa haraka na kutafuta ufumbuzi na utatuzi wa changamoto hiyo ya maji.
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa