• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
Arusha Regional

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Mkoa
      • Chimbuko/Asili ya eneo
      • Orodha ya wakuu wa Mikoa
    • Dira na dhima
    • Maadili ya msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji Mali
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Maji
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
  • Wilaya
    • Arusha
      • Historia
      • Viongozi
    • Arumeru
      • Historia
      • Viongozi
    • Monduli
      • Historia
      • Viongozi
    • Karatu
      • Historia
      • Viongozi
    • Longido
      • Historia
      • Viongozi
    • Ngorongoro
      • Historia
      • Viongozi
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Arusha
    • Halmashauri ya Arusha
    • Halmashauri ya Meru
    • Halmashauri ya Monduli
    • Halmashauri ya Karatu
    • Halmashauri ya Longido
    • Halmashauri ya Ngorongoro
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Ufugaji
    • Kilimo
    • Viwanda
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Ardhi
    • Utalii
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Picha Mbalimbali
    • Habari
    • Matukio

WAZIRI DKT.NDUMBARO AAGIZA TAASISI KUWEKA MIUNDOMBINU ENEO LA KUJENGA UWANJA..

Posted on: December 19th, 2023

Na Elinipa Lupembe.


Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Damas Damian Ndumbaro (MB), ameziagiza Taasisi na Mamlaka za Serikali kusogeza huduma za awali za umeme, maji, barabara na mitandao ya simu kwenye kata ya Olmoth, eneo ambalo linatarajiwa kujengwa uwanja wa mpira, kwa ajili ya mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON).


Waziri Ndumbaro amaetoa maagizo hayo, alipotembelea na kukagua eneo la ujenzi wa mradi huo, na kuweka wazi kuwa, Serikali imepanga mkandarasi kuanza kazi mapema Januari 2024, na kuwaagiza Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini (TARURA), kutengenza miundombinu ya barabara zitakazopitika wakati wote, Mamalaka za Maji kufikisha maji kwenye eneo hilo, TANESCO kufikisha umeme huku TTCL ikitakiwa kufikisha mtandao wa simu eneo hilo wenye kasi ya 5G.


Amezisisitiza taasisi hizo kufanya kazi ndani ya siku 12 zilizosalia na kukamilisha uwekaji wa huduma hizo muhimu, ambazo zitatumiwa na mkandarasi kipindi cha utekelezaji wa ujenzi wa mradi huo, na kuongeza kuwa, mkandarasi atakapofika eneo la mradi akute tayati kuna umeme, maji na barabara zinazopitika kuingia na kutoka.


"Ninawaagiza AUWSA mkandarasi akifika akute maji, kwa ajili ya shughuli za ujenzi, fikisheni miundo mbinu ya maji eneo hili lote, kadhalika TANESCO leteni umeme hapa, TARURA rekebisheni barabara zote, mkandarasi atatakiwa kuleta vitendea kazi 'site' barabara za kuingia na kutoka zipitike muda wote wa utekelezaji wa mradi" Amesisitiza Waziri Dkt.Ndumbaro


Aidha, Dkt. Ndumbaro, ameeleza kuwa, Mhe. Rais Dkt. Samia, ameagiza uwanja huo ujengwe Arusha, kwa lengo maalum, hivyo wananchi wa kata ya Olmoth na Arusha mmepewa heshima kubwa, shirikianeni na Serikali kuhakikisha jambo hili linakamilika kwa kuzingatia maelekezo ya CAF ndani ya miezi 24, uwanja ukabidhiwe kwao, tayari kwa mashindano.


"Ujenzi wa uwanja huu, utaenda sambamba na ujenzi wa miundombinu ya barabara nne za kuingia na kutoka, ujenzi wa viwanja vingine vitatu vya mazoezi na kimoja cha makocha, ujenzi wa maduka na migahawa ya kisasa, uwepo wa internet yenye kasi ya 5G ya bure, miundombinu ambayo itakuza hadhi ya eneo hili pamoja na mkoa wa Arusha kwa ujumla wake" Amesisitiza Dkt. Ndumbaro


Hata hivyo amewapongeza wananvhi wa Arusha, kwa kukubali uwepo wa ujenzi huo, eneo hilo na kuwakumbusha kuwa, wanayo bahati kubwa yabkiwa wenyeji wa mashindano na kuwa uwanja kwako, ungeweza kujengwa mkoa wowote Tanzania, kuchaguliwa Arusha kata ya Olmoth, wananchi hao wanapaswa kushukuru, kuheshimu na kuthamini maamuzi hayo ya Serikali

Awali ziara hiyo iliambatana na makabidhiano ya Hati Miliki ya eneo hilo, ambapo Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. John V.K Mongella, amemkabidhi Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro Hati Miliki ya Eka 39 za awali.


#arushafursalukuki

Tangazo

  • TAZAMA MATOKEO YA MTIHANI WA MOCK MKOA DARASA LA SABA 1 July 06, 2023
  • MATOKEO YA MOCK MKOA DARASA LA SABA 2 July 07, 2023
  • TAZAMA MATOKEO YA MOCK MKOA KIDATO CHA NNE July 07, 2023
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • RC MAKONDA ASHUHUDIA UTIAJI SAINI UJENZI WA BARABARA YA ESO - LONGDON NA UKUMBI WA MIKUTANO ARUSHA.

    April 03, 2025
  • RC MAKONDA ATAKA KUPEWA MAJINA YA WATENDAJI WANAOCHOCHEA MIGOGORO YA KIJAMII.

    March 28, 2025
  • KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA NI MAONO NA MAELEKEZO YA RAIS SAMIA- WAZIRI NDUMBARO.

    March 28, 2025
  • OFISI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI YAFANYIA KAZI MALALAMIKO WANANCHI WA MIANZINI ARUSHA.

    March 28, 2025
  • Angalia Zote

Video

UZINDUZI WA BARABARA YA WASO-SALE
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • SALARY SLIP
  • Taarifa ya Mapato
  • Taarifa za Shule (SIS)
  • Takwimu za Sekta ya Elimu (BEMIS)
  • Video

Viunganishi Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Portal ya Watumishi
  • Takwimu
  • TANAPA

Watembeleaji

world map hits counter

Wasiliana Nasi

Mawaliliano mengine

   

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani
    • Maswali ya Mara kwa Mara

Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa