Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na serikali za Mitaa TAMISEMI Mhe. Mohamed Mchengerwa ameziagiza mamlaka zote za Mikoa na wilaya nchini kuhakikisha kuwa shule zote 26 zinazojengwa maalum kwaajili ya masomo ya Sayansi kwa wasichana zinakamilika kwa wakati na kwa ubora kulingana na thamani ya fedha itakayotumika.
Mhe. Mchengerwa ametoa kauli hiyo leo Septemba 18, 2024 alipoambatana na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda, kukagua maendeleo ya ujenzi wa shule ya Sekondari Longido Samia na kuagiza shule hiyo kukamilika ifikapo Novemba Mosi mwaka huu.
Mhe. Mchengerwa amefikia hatua hiyo mara baada ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Makonda kueleza kuwa ripoti ya awali ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na rushwa Mkoa wa Arusha kubainisha kuwa zaidi ya Shilingi Bilioni 1. 3 utekelezaji wa mradi huo zimetumika nje ya mfumo halali wa matumizi ya fedha za miradi ya maendeleo.
Rc Makonda amesema Shilingi bilioni 1 zilitumika pasipo kupitia mfumo wa kieletroniki wa EFDs lakini pia zaidi ya Shilingi milioni 300 zililipwa bila kuwa na nyaraka za udhibitisho wa kuonesha kuwa zimelipwaje na zinaenda kwa nani ikiwemo ongezeko la asilimia 71 ya fedha iliyotolewa kwaajili ya kulipwa wazabuni kinyume na taratibu.
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa