Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa ameondoka Jijini Arusha kupitia uwanja wa ndege wa Arusha na kuagwa na Mkuu wa Mkoa huo Mhe. Paul Christian Makonda, mara baada ya kumuwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan kwenye maadhimisho ya siku ya maridhiano iliyofanyika leo Februari 26, 2025 kwenye Kituo cha Kimataifa cha mikutano AICC Jijini Arusha.
Wakati wa Maadhimisho hayo, Waziri Mkuu Majaliwa amesisitiza kuwa serikali inatambua na kuthamini kazi zinazofanywa na viongozi wa dini pamoja na wa kimila katika kuhakikisha nchi inakuwa na ustawi wa jamii, akitoa wito kwa Viongozi hao kuendelea kushirikiana na serikali katika kudumisha amani ili watanzania waweze kushiriki kikamilifu katika shughuli za uzalishaji mali.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.