Na Elinipa Lupembe
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa amewasili mkoani Arusha na kupokelewa na Mkuu wa Wilaya ya Monduli Mhe. Festo Shem Kiswaga, kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe.Paul Christian Makonda jioni ya leo Desemba 05, 2024.
Mhe. Majaliwa amefika mkoani Arusha kwa ndege ya shirika la ndege Tanzania (ATC) kupitia Kiwanja cha Ndege Kimataifa Kilimanjaro (KIA).
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa