Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Gerson Msigwa, akizungumza na hadhara ya wananchi waliohudhuria halfa ya kumkabidhi Mkandarasi eneo la kujenga Uwanja wa Mpira wa miguu Arusha, kata ya Olmoti jijini Arusha leo Aprili 06, 2024.
Katibu Mkuu huyo, amesema leo tumekabidhi eneo la ujenzi wa Uwanja wa Mpira wa Arusha kwa Mkandarasi ambaye ni kampuni CRCEG.
Na kuzifafanua Dondoo Muhimu ikiwemo:-
1. Uwanja unajengwa katika eneo la Mirongoine, Kata ya Olmoti ndani ya Jiji la Arusha.
2. Ujenzi utafanyika kwa muda wa miezi 24.
3. Utakuwa kati ya viwanja bora vya mpira Barani Afrika.
4. Utakuwa na uwezo wa kuchukua watazamaji 30,000
5. Utajengwa kwa mchanganyiko wa muonekano wa madini ya Tanzanite, Mlima Kilimanjaro, Eneo la Ngorongoro na Hifadhi ya Serengeti.
6. Utajengwa sambamba na viwanja viwili vya mazoezi na baadaye utaendelezwa kwa kujengwa Bwawa la Kuogelea, viwanja Tenisi, Baskketball na Hosteli.
7. Utawekwa vyumba maalum vya watu mashuhuli (Directors Boxes).
8. Utatumika katika Fainali za AFCON 2027.
Aidha Amemshikuru Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa fursa hii kubwa sana kwa Watanzania.
Awali Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt.Damias Damian Ndumbaro (Mb), amemkabidhi Mkandarasi Eneo la kujenga uwanja huo, hafla iliyofanyika kata ya Olmoti jijini Arusha.
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa