*Awataka watafute kazi nyingine haraka*
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. CPA. Amos Gabriel Makalla, ametoa onyo kwa vijana wanaotumia usafiri wa pikipiki kufanya uhalifu mkoani Arusha, maarufu kama Tatu Mzuka, kuacha mara moja vitendo hivyo badala yake kutafuta kazi nyingine halali ya kufanya.
CPA. Makalla ametoa onyo hilo leo Oktoba 13, 2025 kufuatia malalamiko ya wananchi wa kata ya Muriet wakati, akitembelea na kukagua maendeleo ya mradi wa ujenzi wa Stendi Kuu ya mabasi ya mkoa wa Arusha, kata ya Muriet.
"Tatu mzuka popote walipo, natoa onyo kuachana na uhalifu wa kutumia pikipiki, nasema wasinichokoze, nitakula nao sahani moja, mkoa wa huu unahitaji kuwa salama, nikiwa mkuu wa mkoa ni marufuku Tatu Mzuka, nawaonya watafute kazi nyingine" Amesema CPA Makalla
Aidha, amewasisitiza vijana hao wa Tatu Mzuka kutambua kuwa mkoa wa Arusha una wageni wengi kutoka ndani na nje ya nchi hivyo, hivyo kila mwananchi anatakiwa kufanya kazi halali pamoja na kuwa mlinzi wa usalama wa eneo lake na sio kufanya uhalifu na kuonheza kuwa Arusha inahitajika kuwa salama zaidi.
Hata hivyo, CPA Makalla, amemuagiza Kamanda wa Polisi wa Mkoa, kushughulikia vijana wanatumia pikipiki kufanya vitendo vya uhalifu na kuhakikisha kuwa Arusha sio seheme ya Tatu Mzuka, ili kuhakikisha mkoa unakuwa salama na wananchi waishi kwa amani na utulivu huku wakiendelea kufanya shughuli zao uzalishaji mali kukiwa salama.
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa