Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia,amemzunguzi Hayati Edward Lowassa kuwa ni mtu aliyependa maendeleo ya taifa lake huku akiamini maendeleo huja kwa kuwekeza katika kwa vijana kwa kuwaandaa kwa kuwapa elimu bora itakayowawezesha kujikwamua kijamii na kiuchumi.
Mhe. Rais amesema hayo, wakati akizungumza na maelfu ya waombolezaji walishiriki ibada ya mazishi ya Hayati Edward Lowassa, yaliyofanyika Kijiji cha Ngarash wilaya ya Monduli Februari, 17, 2024.
Dkt. Samia amesema kuwa Hayati Lowasa aliamini kila kijana akipata elimu itampa ujuzi na maarifa na kuwa na stadi zitakazomuwezesha kumudu kujitegemea na kulitumikia taifa lake ndio maana alisimamia kipaumbele chake cha Elimu, Elimu,Elimu.
Lowasa alipenda vijana wapate ujuzi na maarifa ndio maana alipokuwa mgombea Urais katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 aliweka wazi kipaumbele chake cha kwanza elimu, cha pili ni elimu cha tatu pia ni elimu.
Lowassa alikuwa muumini wa elimu, kama nyenzo ya kujikwamua kutoka katika umasikini na mara zote alisistiza kuwa, aliuchukia umasikini na kusisitiza umuhimu wa elimu bora kwa wote, elimu itakayowaandaa vijana kuingia kwenye ushindani wa soko la ajira duniani.
"Matunda ya dhamira ya Lowassa ya kusimamia sekta ya elimu ndio yanayoonekana sasa, kwa kuimarika kwa sekta ya elimu na ongezeko la shule za sekodandari na idadi ya wanafunzi nchini" Ameweka wazi Rais Samia
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa