• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
Arusha Regional

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Mkoa
      • Chimbuko/Asili ya eneo
      • Orodha ya wakuu wa Mikoa
    • Dira na dhima
    • Maadili ya msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji Mali
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Maji
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
  • Wilaya
    • Arusha
      • Historia
      • Viongozi
    • Arumeru
      • Historia
      • Viongozi
    • Monduli
      • Historia
      • Viongozi
    • Karatu
      • Historia
      • Viongozi
    • Longido
      • Historia
      • Viongozi
    • Ngorongoro
      • Historia
      • Viongozi
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Arusha
    • Halmashauri ya Arusha
    • Halmashauri ya Meru
    • Halmashauri ya Monduli
    • Halmashauri ya Karatu
    • Halmashauri ya Longido
    • Halmashauri ya Ngorongoro
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Ufugaji
    • Kilimo
    • Viwanda
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Ardhi
    • Utalii
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Picha Mbalimbali
    • Habari
    • Matukio

NCHI ZA AFRIKA ZAHIMIZWA KUANDAA MTAJI WA RASILIMALIWATU KWA AJILI YA KARNE YA 21

Posted on: August 13th, 2024

Na Elinipa Lupembe 


Nchi za Afrika zimetakiwa kujenga mtaji wa Rasilimali watu kwa ajili ya karne ya 21, kwa kutoa elimu inayohusu mafunzo jumuishi ya kudumu katika maisha yanayoendana na changamoto za nchi zao, kuendana na mabadiliko ya kidijitali kisayansi na kiteknolojia.


Rai hiyo imetolewa na Makamu wa Rais Jamhuri ya Muungano Tanzania Mhe. Dkt.Philip Isdor Mpango wakati akifungua Kongamano la Elimu kwa nchi za Ukanda wa Afrika Mashariki na Maadhimisho  ya mwaka wa Elimu wa Umoja wa Afrika, kongamano linalofanyika mkoani Arusha  kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC), Ukumbi wa Simba Agosti 13, 2024.


Amesema kuwa nchi ya Tanzania imefanya mapitio katika mfumo wa elimu kwa kufanya mabadiliko ya mitaala ya elimu na kufanikiwa kugawanya elimu ya sekondari katika mikondo miwili, ikilenga elimu ya jumla na elimu ya ufundi stadi.


Aidha, ameweka wazi kuwa, mabadiliko hayo ya mfumo wa elimu yamelenga kuboresha ubora wa elimu  katika mabadiliko ya kidijitali na mambo mapya ya kiteknolojia ndani ya mfumo wa elimu, ambapo wapo wanafunzi watahitimu na cheti cha shule ya sekondari na wengine cheti cha mafunzo ya ufundi stadi.


"Tunafanya hivi ili kuhakikisha kuwa mfumo wetu wa elimu unatoa fursa za kutosha kwa wale wanafunzi ambao uwezo wao uko zaidi kwenye ujuzi badala ya taaluma ya Fauci tulifanya hivyo kwa kutambua ukweli kwamba moja ya kikwazo cha kuvutia uwekezaji katika nchi yetu ni ukosefu wa ujuzi wa kutosha." 


Hata hivyo amebainisha kuwa, maboresho hayo yatahusisha uwekezaji katika mazingira ya kufundishia na kujifunzia katika uboreshaji wa miundombinu ya elimu ili kuhakikisha watoto wote wanapata fursa ya kupata elimu inaoyendana na ongezeko la idadi ya  walimu na upatikanaji wa vifaa vya kufundishia na kujifunzia vya kidijitali.


Licha ya kuwa lengo ni kuboresha ubora lakini zaidi ni kuhakikisha kuwa elimu inampa mwananfunzi ujuzi na maarifa yanayoendana na ulimwengu wa utandawazi na maendeleo ya haraka ya kiteknolojia.


Tangazo

  • TAZAMA MATOKEO YA MTIHANI WA MOCK MKOA DARASA LA SABA 1 July 06, 2023
  • MATOKEO YA MOCK MKOA DARASA LA SABA 2 July 07, 2023
  • TAZAMA MATOKEO YA MOCK MKOA KIDATO CHA NNE July 07, 2023
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • RC MAKONDA ASHUHUDIA UTIAJI SAINI UJENZI WA BARABARA YA ESO - LONGDON NA UKUMBI WA MIKUTANO ARUSHA.

    April 03, 2025
  • RC MAKONDA ATAKA KUPEWA MAJINA YA WATENDAJI WANAOCHOCHEA MIGOGORO YA KIJAMII.

    March 28, 2025
  • KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA NI MAONO NA MAELEKEZO YA RAIS SAMIA- WAZIRI NDUMBARO.

    March 28, 2025
  • OFISI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI YAFANYIA KAZI MALALAMIKO WANANCHI WA MIANZINI ARUSHA.

    March 28, 2025
  • Angalia Zote

Video

UZINDUZI WA BARABARA YA WASO-SALE
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • SALARY SLIP
  • Taarifa ya Mapato
  • Taarifa za Shule (SIS)
  • Takwimu za Sekta ya Elimu (BEMIS)
  • Video

Viunganishi Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Portal ya Watumishi
  • Takwimu
  • TANAPA

Watembeleaji

world map hits counter

Wasiliana Nasi

Mawaliliano mengine

   

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani
    • Maswali ya Mara kwa Mara

Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa