Karibu Tawala wa Mkoa wa Arusha Dkt. Athumani Kihamia amewataka maafisa TEHEMA kuendelea kutumia mashine za kukusanya mapato(POS) katika maeneo yao.
Ameyasema hayo alipokuwa akifungua mafunzo ya matumizi ya mashine za kukusanya mapato (POS) kwa ngazi ya Mikoa na Halmashauri kutoka Mikoa 4 ya Kanda ya Kaskazini, Jijini Arusha.
Amewataka wakahakikishe fedha zote zinazokusanywa na mfumo huo zinawekwa benki kwa wakati.
Aidha, amekemea vikali vitendo vya baadhi ya wakusanya mapato kutoka ngazi za msingi na kwenye vituo mbalimbali vya kukusanya mapato hayo kutokuwa waaminifu kwa kutopeleka fedha wanazokusanya benki kwa wakati, au zikiwa pungufu na wengine kutopeleka kabisa.
Dkt. Kihamia amewataka maafisa hao kuhakikisha wanapata elimu ya kutatua changamoto zote hizo ili wanaporudi kwenye vituo vyao vya kazi wakazitatue kwa haraka zaidi.
Akizungumzia lengo kubwa la mafunzo hayo Mkurugenzi wa TEHEMA kutoka ofisi ya Rais TAMISEMI Erick Kitali amesema, mafunzo hayo yatakuwa niyakukumbushana majukumu ya maafisa TEHEMA hao ili wasiingiliane na taaluma vyingine katika utendaji wao wa kazi.
Pia, watafundisha namna ya kutatua changamoto za udanganyifu katika ukusanyaji wa mapato kwa kutumia mfumo huo wa POS.
Mafunzo hayo yamejumuisha maafisa TEHEMA 211 kutoka ya Arusha, Tanga, Kilimanjaro na Manyara pamoja na Halmashauri zake na yanatarajiwa kufanyika kwa siku 2.
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa