• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
Arusha Regional

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Mkoa
      • Chimbuko/Asili ya eneo
      • Orodha ya wakuu wa Mikoa
    • Dira na dhima
    • Maadili ya msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji Mali
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Maji
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
  • Wilaya
    • Arusha
      • Historia
      • Viongozi
    • Arumeru
      • Historia
      • Viongozi
    • Monduli
      • Historia
      • Viongozi
    • Karatu
      • Historia
      • Viongozi
    • Longido
      • Historia
      • Viongozi
    • Ngorongoro
      • Historia
      • Viongozi
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Arusha
    • Halmashauri ya Arusha
    • Halmashauri ya Meru
    • Halmashauri ya Monduli
    • Halmashauri ya Karatu
    • Halmashauri ya Longido
    • Halmashauri ya Ngorongoro
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Ufugaji
    • Kilimo
    • Viwanda
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Ardhi
    • Utalii
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Picha Mbalimbali
    • Habari
    • Matukio

RC MAKALLA AITAKA TUME YA TAIFA YA UMWAGILIAJI KUFANYA MAAMUZI KWA MKANDARASI BWAWA LA EYASI...

Posted on: September 23rd, 2025

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. CPA Amos Gabriel Makalla ameitaka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji kufanya maamuzi na majadiliano ya haraka na Mkandarasi Tunnel Sadd Ariana kutoka Nchini Iran anayetekeleza ujenzi wa Bwawa la Eyasi Wilayani Karatu, ili kujua hatma ya utekelezaji wa mradi huo unaosuasua kwa kipindi kirefu.


Mhe. Makalla amebainisha hayo Jumanne Septemba 23, 2025 alipofanya ziara ya kukagua utekelezaji wa mradi huo, akionesha kusikitishwa na kusuasua kwake ambapo mpaka sasa mradi huo umefikia asilimia nne pekee ya utekelezaji wake ilihali ulitakiwa kuwa umefikia asilimia 90 kufikia hivi sasa huku pande zote za Mkandarasi na Tume wakiwa na sababu tofauti kama sehemu ya vikwazo vinavyokwamisha utekelezaji wake.


"Mimi kama Mkuu wa Mkoa na Mwenyekiti wa Kamati ya usalama nishauri na kupendekeza kwa Tume kwamba mkae na Mkandarasi kama hana sifa ya kuendelea ni bora mkawa na makubaliano ya pande zote mbili tukaachana na tukatafuta Mkandarasi mwingine. Wananchi wana matarajio na mradi huu hivyo jambo hili lifanyike kwa haraka." Amesema Mhe. Makalla akisisitiza kuzingatiwa kwa taratibu za kisheria katika majadiliano yao.


Awali katika maelezo yake, Mhe. Mkuu wa Mkoa akizungumza na Maofisa wa Tume ya Umwagiliaji pamoja na Wakandarasi hao ameeleza kuwa serikali imetenga Bilioni 21 na Milioni 831 katika kutekeleza mradi wa bwawa hilo ili kuondoa changamoto ya mafuriko kwenye Kata za Mang'ola na Baray za Wilayani Karatu Mkoani  Arusha pamoja na kuzisaidia Kata hizo katika kuimarisha Kilimo cha Umwagiliaji.


Kwa upande wake Bw. Leopard Lunji, Mkurugenzi wa Idara ya miundombinu kutoka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji amemueleza Mhe. Makonda kuwa ndani ya wiki mbili zijazo wataketi na Mkandarasi huyo ili kufanya makubaliano ya pamoja katika kutekeleza maagizo na maelekezo ya Mhe. Makalla ili wananchi waweze kunufaika na mradi huo kwa wakati.

Tangazo

  • TAZAMA MATOKEO YA MTIHANI WA MOCK MKOA DARASA LA SABA 1 July 06, 2023
  • MATOKEO MTIHANI WA UTAMIRIFU (MOCK) 2025 DARASA LA SABA (VII)- MKOA WA ARUSHA June 07, 2025
  • MATOKEO YA MOCK MKOA DARASA LA SABA 2 July 07, 2023
  • TAZAMA MATOKEO YA MOCK MKOA KIDATO CHA NNE July 07, 2023
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • RC MAKALLA: UFUNGUZI TAWI LA CRDB NAMANGA UTACHOCHEA BIASHARA NA UCHUMI WA WANANCHI WA MPAKANI ..

    September 26, 2025
  • RC MAKALLA ATAKA MPANGO MKAKATI WA UTALII UKIJUMUISHA FURSA NA MAANDALIZI YA AFCON 2027...

    September 25, 2025
  • WANANCHI WALIOLALAMIKIA MGAO WA MAJI WAFURAHIA UJENZI WA TENKI JIPYA LA MAJI...

    September 24, 2025
  • RC MAKALLA: ARUSHA ITAENDELEA KUWA NA AMANI SASA NA HATA  BAADA YA UCHAGUZI...

    September 24, 2025
  • Angalia Zote

Video

UZINDUZI WA BARABARA YA WASO-SALE
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • SALARY SLIP
  • Taarifa ya Mapato
  • Taarifa za Shule (SIS)
  • Takwimu za Sekta ya Elimu (BEMIS)
  • Video

Viunganishi Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Portal ya Watumishi
  • Takwimu
  • TANAPA

Watembeleaji

world map hits counter

Wasiliana Nasi

Mawaliliano mengine

   

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani
    • Maswali ya Mara kwa Mara

Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa