• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
Arusha Regional

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Mkoa
      • Chimbuko/Asili ya eneo
      • Orodha ya wakuu wa Mikoa
    • Dira na dhima
    • Maadili ya msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji Mali
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Maji
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
  • Wilaya
    • Arusha
      • Historia
      • Viongozi
    • Arumeru
      • Historia
      • Viongozi
    • Monduli
      • Historia
      • Viongozi
    • Karatu
      • Historia
      • Viongozi
    • Longido
      • Historia
      • Viongozi
    • Ngorongoro
      • Historia
      • Viongozi
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Arusha
    • Halmashauri ya Arusha
    • Halmashauri ya Meru
    • Halmashauri ya Monduli
    • Halmashauri ya Karatu
    • Halmashauri ya Longido
    • Halmashauri ya Ngorongoro
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Ufugaji
    • Kilimo
    • Viwanda
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Ardhi
    • Utalii
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Picha Mbalimbali
    • Habari
    • Matukio

WAKULIMA MANG'OLA WAMSHUKURU RAIS SAMIA KWA MRADI WA UMWAGILIAJI...

Posted on: September 22nd, 2025

_Rc Makalla ataja Mapinduzi makubwa ya kiuchumi kwa wananchi akiagiza mradi ukamilike haraka_


Wananchi wa Vijiji saba vya Kata za Mang'ola na Baray Wilayani Karatu Mkoani Arusha wamemshukuru Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa utekelezaji wa ujenzi wa mradi mkubwa wa skimu za Umwagiliaji za bonde la Eyasi, Mradi wenye kugharimu  Shilingi Bilioni 38, 434, 137, 621. 18, wakisema mradi huo umekuwa na manufaa makubwa katika kuongeza tija na uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara katika eneo hilo.


Wakati wa ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. CPA Amos Gabriel Makalla leo Jumanne Septemba 23, 2025, wakati wa ukaguzi wa mradi huo, wananchi hao wameeleza pia namna ambavyo wamenufaika na ruzuku za mbolea na pembejeo za kilimo, wakisema maendeleo ya Kata zao kwasasa na ukuaji wa uchumi unaoshuhudiwa umetokana na tija kubwa wanayoipata kwenye kilimo cha Vitunguu, Mpunga na mahindi.


Akizungumza mbele ya Mkuu wa Mkoa, Bw. Joseph Hitla, Mkazi na Mkulima wa Kijiji cha Maleckchand amemshukuru pia Mhe. Makalla kwa kusimamia vyema utekelezaji wa shughuli za serikali katika eneo hilo pamoja na kuwatembelea kwenye mashamba yao, akisema Mhe. Makalla amekuwa Mkuu wa Mkoa wa kwanza kutembelea mashamba hayo na kukagua shughuli za kilimo zinazoendelea katika eneo hilo.


Kulingana na CPA Makalla, kukamilika kwa mradi huo kutawanufaisha wananchi wa Vijiji vya Mang'ola Barazani, Maleckchand, Laghangarer pamoja na Vijiji vya Qang'dend, Mbuga nyekundu, Jobaj na Dumbechand, akiagiza Mkandarasi na Tume ya Taifa ya Umwagiliaji kuongeza kasi kuhakikisha mradi huo unakamilika ndani ya muda uliopangwa Kimkataba.


Mradi wa skimu za umwagiliaji Bonde la Eyasi unatekelezwa na Mkandarasi M/S CRJE (EA) Ltd wakiingia makubaliano na Tume ya Taifa ya Umwagiliaji mnamo Machi 30, 2023 kwa Mkataba wa miezi 18 ya kiutekelezaji, mradi ukitarajiwa kukamilika na kukabidhiwa rasmi serikalini kufikia Machi Mosi mwaka 2026.


Tangazo

  • TAZAMA MATOKEO YA MTIHANI WA MOCK MKOA DARASA LA SABA 1 July 06, 2023
  • MATOKEO MTIHANI WA UTAMIRIFU (MOCK) 2025 DARASA LA SABA (VII)- MKOA WA ARUSHA June 07, 2025
  • MATOKEO YA MOCK MKOA DARASA LA SABA 2 July 07, 2023
  • TAZAMA MATOKEO YA MOCK MKOA KIDATO CHA NNE July 07, 2023
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • RC MAKALLA: UFUNGUZI TAWI LA CRDB NAMANGA UTACHOCHEA BIASHARA NA UCHUMI WA WANANCHI WA MPAKANI ..

    September 26, 2025
  • RC MAKALLA ATAKA MPANGO MKAKATI WA UTALII UKIJUMUISHA FURSA NA MAANDALIZI YA AFCON 2027...

    September 25, 2025
  • WANANCHI WALIOLALAMIKIA MGAO WA MAJI WAFURAHIA UJENZI WA TENKI JIPYA LA MAJI...

    September 24, 2025
  • RC MAKALLA: ARUSHA ITAENDELEA KUWA NA AMANI SASA NA HATA  BAADA YA UCHAGUZI...

    September 24, 2025
  • Angalia Zote

Video

UZINDUZI WA BARABARA YA WASO-SALE
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • SALARY SLIP
  • Taarifa ya Mapato
  • Taarifa za Shule (SIS)
  • Takwimu za Sekta ya Elimu (BEMIS)
  • Video

Viunganishi Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Portal ya Watumishi
  • Takwimu
  • TANAPA

Watembeleaji

world map hits counter

Wasiliana Nasi

Mawaliliano mengine

   

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani
    • Maswali ya Mara kwa Mara

Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa