• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
Arusha Regional

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Mkoa
      • Chimbuko/Asili ya eneo
      • Orodha ya wakuu wa Mikoa
    • Dira na dhima
    • Maadili ya msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji Mali
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Maji
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
  • Wilaya
    • Arusha
      • Historia
      • Viongozi
    • Arumeru
      • Historia
      • Viongozi
    • Monduli
      • Historia
      • Viongozi
    • Karatu
      • Historia
      • Viongozi
    • Longido
      • Historia
      • Viongozi
    • Ngorongoro
      • Historia
      • Viongozi
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Arusha
    • Halmashauri ya Arusha
    • Halmashauri ya Meru
    • Halmashauri ya Monduli
    • Halmashauri ya Karatu
    • Halmashauri ya Longido
    • Halmashauri ya Ngorongoro
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Ufugaji
    • Kilimo
    • Viwanda
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Ardhi
    • Utalii
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Picha Mbalimbali
    • Habari
    • Matukio

WATALII MAARUFU KUPANDA MILIMA MIREFU DUNIANI; WAWASILI NCHINI KUSHIRIKI TAMASHA LA KUPANDA MLIMA KILIMANJARO...

Posted on: December 27th, 2023


Kundi la Watalii maarufu wa kupanda milima mirefu Duniani kutoka nchini China, wamewasili mkoani Arusha na kupokelewa na Mkuu wa Mkoa huo Mhe. John V.K Mongella, na

kufanya mazungumzo pamoja na kushiriki chakula cha jioni, hafla iliyofanyika kwenye hoteli ya Mount Meru, jijini Arusha,  jioni ya leo tarehe 26 Desemba, 2023.


Kundi hilo likiwa na jumla ya  Watalii 54, likongozwa na Ndugu. Xia Boyu, wako nchini kwa ajili ya kushiriki Tamasha la Kupanda Mlima Kilimanjaro, lililoandaliwa na Kampuni ya kitanzania ya Gosheni Safaris.


Akizungumza wakati wa hafla ya kuwapokea watalii hao, Mhe. Mongella ameeleza kuwa, ujio wa wageni hao umetokana  na uhusiano mzuri uliopo kati ya nchi ya Tanzania na China, uhusiano ambao ulitengenezwa na waasisi wa mataifa hayo na kuendelezwa na viongozi waliopo sasa.


“Nichukue fursa hii kuwakaribisha Tanzania, kushiriki Tamasha la Kupanda Mlima Kilimanjaro, ukiwa ndio  msimu mzuri wa kupanda mlima Kilimanjaro, ninaamini mtafurahia muonekano na mandari nzuri ya mlima huo mrefu Afrika" Amesema Mhe. Mongella.


Aidha ameipongeza Kampuni utalii ya Goshen safaris, kwa kundaa Tamasha  hilo, ambalo ni muhimu na lenye manufaa kwa nchi ya Tanzania na nchi nyingine, ikiwemo China.


Amefafanua kuwa, msimu wa mwisho wa mwaka, ni msimu mzuri zaidi kwa kupanda mlima Kilimanjaro,  hali itakayowafanya kufurahia mandari nzuri ya mlima na kuweza kuitangaza Tanzania kupitia mlima huo wa Kilimanjaro


Katika hafla, hiyo, Mkuu huyo wa Mkoa licha ya kuwakaribisha watalii hao, amewapatia vyeti ya kuwapongeza wapanda mlima hao maarufu dunia,ambao wamekwishapanda mlima mrefu zaidi duniani Everest Zaidi ya mara 10.


Naye Kiongozi wa Watalii hao, Xia Boyu, amekiri kufurahishwa na  uwepo wao nchini pamoja na kuvutiwa na mandhari nzuri ya mkoa wa Arusha, huku akiamini safari yao ya siku 10 itakuwa nzuri na ya furaha kwa wote.


"Tumefurahi kuwa Tanzania, Tanzania ni nchi nzuri, watu wake ni wazuri wana upendo, safari yetu itakuwa nzuri na ya furaha, tunafuhia kupanda Mlima Kilimanjaro lakini tunafurahi zaidi kushiriki Tamasha hili kubwa" Amesema Boyu


Awali, Wageni hao wapo nchini kwa siku 10, wakitumia siku 7 kupanda mlima Kilimanjaro na siku 3 kwaajili ya safari, huku Kundi likiwa ni maarufu duniani kwa kupanda mlima Mrefu zaidi, wakiwa tayari wamepanda mlima Everest zaidi ya mara 10, mlima ambao ni wa kwanza kwa urefu duniani.


Ikumbukwe kuwa, ujio wa watalii hao ni matokea ya Filamu ya Royal Tour, iliyochezwa na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hasaan, ikiwa ni mkakati wa kutangaza utalii ndani ja nje ya nchi.

#Arushafursalukuki

Tangazo

  • TAZAMA MATOKEO YA MTIHANI WA MOCK MKOA DARASA LA SABA 1 July 06, 2023
  • MATOKEO YA MOCK MKOA DARASA LA SABA 2 July 07, 2023
  • TAZAMA MATOKEO YA MOCK MKOA KIDATO CHA NNE July 07, 2023
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • RC MAKONDA ASHUHUDIA UTIAJI SAINI UJENZI WA BARABARA YA ESO - LONGDON NA UKUMBI WA MIKUTANO ARUSHA.

    April 03, 2025
  • RC MAKONDA ATAKA KUPEWA MAJINA YA WATENDAJI WANAOCHOCHEA MIGOGORO YA KIJAMII.

    March 28, 2025
  • KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA NI MAONO NA MAELEKEZO YA RAIS SAMIA- WAZIRI NDUMBARO.

    March 28, 2025
  • OFISI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI YAFANYIA KAZI MALALAMIKO WANANCHI WA MIANZINI ARUSHA.

    March 28, 2025
  • Angalia Zote

Video

UZINDUZI WA BARABARA YA WASO-SALE
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • SALARY SLIP
  • Taarifa ya Mapato
  • Taarifa za Shule (SIS)
  • Takwimu za Sekta ya Elimu (BEMIS)
  • Video

Viunganishi Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Portal ya Watumishi
  • Takwimu
  • TANAPA

Watembeleaji

world map hits counter

Wasiliana Nasi

Mawaliliano mengine

   

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani
    • Maswali ya Mara kwa Mara

Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa