Kwa kipindi cha Julai 2021 mpaka Machi, 2022 jumla ya wananchi (Watalii wa ndani), 167,173 walitembelea vivutio mbalimbali vya utalii vilivyopo katika Mkoa wa Arusha hii ni kutokana na juhudi za Mkoa kuhamasisha wananchi kuhusu umuhimu wa utalii wa ndani. Jumla ya Watalii wa nje wapatao 163,062 walitembelea vivutio mbalimbali vya utalii vilivyo ndani ya Mkoa, jumla ya watalii 10,526 walitembelea maeneo ya malikale. Aidha, Jumla ya maeneo mapya 2 yenye fursa za utalii yamebainishwa katika Halmashauri ya Meru na jumla ya vikundi 11 vya vijana vimeanzishwa na kupewa elimu bora ya namna ya kuanzisha kampuni za kutembeza na kuongoza watalii.
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa