Halmashauri zimeshatoa jumla ya fedha shilingi bilioni 1.229 kama mikopo kwenye vikundi 197 vya ujasilimali vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu ambazo zimezalisha ajira nyingi kwa wananchi na shughuli zake zimeongeza kipato.
Mpango kunusuru kaya maskini (TASAF) imeendelea kuwasaidia wananchi maskini katika mkoa mzima. TASAF-Fedha za ruzuku kwa kaya masikini zimeongezeka kutoka shilingi bilioni 1.395 mwaka 2020 hadi kufikia shilingi bilioni 2.488 mwaka 2021, Katika kipindi hicho, Mkoa umefanikiwa kuandikisha Vijiji/Mitaa mipya 294 ambayo haikuwa kwenye Mpango wa TASAF na jumla ya kaya mpya 31,665 zimeandikishwa na zitanufaika na mpango wa TASAF.
Matokeo chanya yaliyopatikana katika kipindi hiki, ni kwamba walengwa wameweza kuanzisha shughuli mbalimbali za ujasiriamali kama ufugaji, kilimo na biashara ndogondogo ambazo zimawawezesha kuwa na uhakika wa chakula, malazi na mavazi.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.