Ofisi ya Meneja Wakala wa Barabara (TANROADS) Mkoa wa Arusha inahudumia jumla ya Km 581.14 za Barabara Kuu (Trunk roads) na km. 895.31 Barabara za Mkoa (Regional roads). Kati ya hizo, Km 425.35 ni barabara za lami sawa na asilimia 29.8 na sehemu iliyobaki yenye Km 1051.10 sawa na asilimia 70.2 ni barabara za changarawe. Barabara Kuu (Trunk Roads) zina jumla ya Km 582.7 ambazo kati ya hizo, Km 368.04 sawa na asilimia 63.3 ni za kiwango cha lami, na Km 213.1 zilizobaki sawa na asilimia 36.70 ni za changarawe/udongo. Aidha, Barabara za Mkoa (Regional Roads) zina jumla ya Km 895.31 kati ya hizo Km 57.31 sawa na asilimia 6.40 ni barabara za lami na Km 838.00 sawa na asilimia 93.60. ni za changarawe/ udongo. Aidha, urefu wa barabara umeendelea kuongezeka kutoka 1476.45km 2020 hadi km 1494.45 kutokana na urefu km 18.0 kupandishwa hadhi (gazetted). (Barabara ya Mianzini-Timbolo (18 km).
Serikali imeendelea kuimarisha barabara nchini zinazounganisha nchi yetu na nchi Jirani, Makao Makuu ya Mkoa na Makao Makuu ya Wilaya kwa barabara zinazopitika kwa wakati wote.
Katika kipindi cha mwaka wa fedha 2021/22 kiasi cha shilingi milioni 7207.54 kilitengwa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya barabara inayosimamiwa na TANROADS Mkoa wa Arusha. Ambapo hadi kufikia mwezi Machi, 2022 kiasi cha shilingi milioni 420.86 kilipokelewa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya Kijenge -Usa River, Minazini-Ngaramtoni, Longido-Oldonyolengai, Tengeru-Merereni na Kia-Majengo na kiasi cha shilingi milioni 415.104 kilitumika kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya Kijenge -Usa River na Kia-Majengo.
Mafanikio yaliyopatika katika matengenezo ya barabara za katika kipindi cha mwaka mmoja wa Serikali ya awamu ya Sita ni kama ifuatavyo:
Barabara yenye urefu wa Kilometa 49 katika Barabara ya Mto wa Mbu-Loliondo (217km) imejengwa kwa kiwango cha lami imekamilika kutoka Wasso hadi Sale umefikia asilimia 97 % na inatumika. Barabara hii imejengwa kwa kiwango cha lami kwa gharama ya shilingi bilioni 87.3
Ujenzi wa Mzani wa kisasa wa kupima magari yakiwa kwenye mwendo katika eneo la Kimokouwa barabara ya Arusha hadi Namanga umekamilika kwa asilimia mia 100 na magari yanapimwa yakiwa katika mwendo.
Miradi inayotekelezwa na Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini (TARURA)
TARURA- Kwa mwaka wa fedha 2020/2021 hadi kufikia Februari 2022 Mkoa wa Arusha umetekeleza asilimia 90.86 ya miradi yote.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.