Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda ameliagiza Jeshi la Polisi wilqya ya Arumeru kukamkanata Afisa Ardhi Mteule halmashauri ya Arusha, Shednevenaz Mwakyokola kwa tuhuma za kupokea rushwa ya shilingi milioni 5 siku chache zilizopita mbele ya mamcho yake.
Mhe.Makonda ametoa agizo hilo ambalo tayari limetekelezwa na Jeshi hilo la Polisi, wakati wa Mkutano wa Hadhara wa kusikiliza kero za wananchi wa halmashauri hiyo, uliofanyika kwenye uwanja wa kanisa Katholiki Ngaramtoni Mei 28, 2024, ikiwa ni wilaya ya nne ya zaira yake ya 'Siku 6 za Moto Arusha' ya kukagua utekelezaji wa shughuli za maendeleo katika mkoa wa Arusha.
Mhe. Makonda ameeeza namna alivyoshuhudia Mteule huyo akipokea rushwa ya shilingi milioni 5 eneo la Kituo cha Mikutano ya Kimataifa Arusha, siku ambayo kulikuw ana ugeni wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Dkt. Ali Hassan Mwinyi Arusha na kuitupa bahasha yenye pesa hizo mara alipogundua Mkuu huyo amemuona.
Hata hivy, Mhe. Makonda ameigaza TAKUKURU wilaya ya Arumeru na Mkoa wa Arusha kuongeza kasi ya kufanya kazi kwa kuwa wilaya ya Arumeru inanuka rushwa na kuwataka viongozi na watendaji wa Serikali kufanya kazi kwa uadilifu kwa kuzingatia maadili ya utumishi wa Umma huku kipaumbele chao kikiwa ni kuwahudumia wannachi na kutatua kero na changamoto zinazowakabili na si vinginevyo
"Sisi watumishi wa Umma tunalipwa mishahara kwa kodi za wananachi, wananchi ndio wametuajiri hawa ndio 'maboss' wetu, tunalojukumu la kuwahudumia, kila mtumishi kwa nafasi yake anapaswa kuwajibika kwa wananchi hawa, tusiwanyanyase" Amesisitiza Mhe. Makonda.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.