Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda ametangaza kuwa Disemba 09, 2024 wakati Tanzania itakapokuwa inaadhimisha Miaka 63 ya Uhuru, Mkoani Arusha kutafanyika Kongamano kubwa la maombi la kuombea Mkoa wa Arusha dhidi ya changamoto mbalimbali zilizopo.
Mhe. Paul Christian Makonda ametoa kauli hiyo leo Novemba 19, 2024 alipokutana na Viongozi wa madhehebu mbalimbali ya dini mkoani Arusha, akisema kutafanyika pia matembezi maalum ndani ya Jiji la Arusha yakijumuisha Viongozi hao wa dini na wananchi wa mkoa wa Arusha.
"Tutatembea kwa pamoja maeneo mbalimbalimkoani Arusha tukiwa na bendera, tukitamka maneno ya baraka na maombezi kwa Mkoa wetu wa Arusha tukiombea amani, baraka, biashara zetu pamoja na kizazi tukitakacho mkoani Arusha." Amesema Mhe. Makonda.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.