Mkoa wa Arusha umepewa dhamana ya kusimamia maadhimisho ya mpango harakishi na shirikishi awamu ya pili ya uhamasishaji na utoaji wa chanjo ya UVIKO 19 Kitaifa.
Akizungumza katika semina elekezi kwa waratibu wa elimu Afya ngazi ya Mkoa,wahudumu wa Afya ngazi ya jamii,viongozi kutoka Wizara mbalimbali kutoka mikao 26 na waandishi wa habari, Mganga Mkuu wa Serikali Dkt. Aifello Wedson Sichalwe amesema bado nguvu kubwa inaitajika katika kuwafikia wananchi wengi katika utoaji wa chanjo.
Kwani bado maambukizi ya UVIKO 19 yapo na Jamii inatakiwa kuendelea kuchukua tahadhari ya kujikinga kwa kufuata taratibu zote.
Mkurugenzi wa huduma ya kinga kutoka Wizara ya Afya Dkt. Beatrice Mutayoba amesema lengo la mafunzo hayo ni kujengeana uwelewa wa namna ya kuendelea kuhamasisha utoaji wa chanjo katika Jamii.
Ugonjwa wa UVIKO 19 uligundulika rasmi duniani mnamo Disemba 19 na nchini Tanzania ulifika Machi 16, 2020 na mpaka sasa jumla ya watu 973,728 sawa na asilimia 92 wameshachanja na dozi zilizokwisha ingia nchini ni 4,421,540.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.