• Complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Arusha Regional

The United Republic of Tanzania President Office Regional Administration and Local Government Arusha Regional

  • Home
  • About Us
    • History
      • Chimbuko/Asili ya eneo
      • Orodha ya wakuu wa mikoa waliopita-Arusha
    • Dira na dhima
    • The basics
    • Strategies
  • Administration
    • Structure
    • Departments
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji Mali
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Maji
    • Units
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
  • District
    • Arusha
      • Historia
      • Viongozi
    • Arumeru
      • Historia
      • Viongozi
    • Monduli
      • Historia
      • Viongozi
    • Karatu
      • Historia
      • Viongozi
    • Longido
      • Historia
      • Viongozi
    • Ngorongoro
      • Historia
      • Viongozi
  • Councils
    • Arusha CC
    • Arusha DC
    • Meru DC
    • Monduli DC
    • Karatu DC
    • Longido DC
    • Ngorongoro DC
  • Investment Opportunities
    • Tourism
    • Livestock
    • Agricultre
    • Industrial
  • Our Service
    • Health
    • Education
    • Water
    • Land
    • Tourism
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Acts
    • Application Forms
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
    • Speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events

ARUSHA MBIONI KUFANYWA KUWA KITOVU CHA UTALII WA MATIBABU UKANDA WA AFRIKA MASHARIKI.

Posted on: January 10th, 2025

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda na Waziri wa Afya nchini Tanzania Mhe. Jenista Mhagama, wamekubaliana kukutana Dodoma Makao Makuu ya Wizara hiyo, kufanya mazungumzo ya pamoja ya kupanga utekelezaji wa ndoto na Maono ya Mhe. Makonda ya kuufanya Mkoa wa Arusha kuwa Kitovu cha Utalii wa Matibabu kwa Ukanda wa Afrika ya Mashariki.



Wakati wa Mazungumzo yao Makao makuu ya Mkoa Jijini Arusha, Mhe. Makonda amemueleza Waziri Mhagama kuwa Mkoa unatekeleza kwa kasi agizo la Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan la kukuza utalii wa aina mbalimbali Mkoani hapa, akisema kupatikana kwa Hospitali itakayokuwa na Huduma za kibingwa na Kibobezi sambamba na madaktari bingwa kutoka ndani na nje ya nchi, kutasaidia kuwavuta watu wanaoizunguka Tanzania na Raia wa kigeni kusafiri kufuata matibabu hayo Mkoani Arusha na hivyo kukuza utalii na kusisimua pato la Mkoa wa Arusha.



Waziri Mhagama, Kando ya Kumshukuru Mhe. Makonda kwa kusimamia vyema utoaji huduma za kiafya Mkoani Arusha ikiwemo Programu ya Kliniki yake ya afya iliyofanyika mwaka 2024, amemuahidi kuwa atamuita Jijini Dodoma, kujadiliana pamoja Mkakati madhubuti wa kutekeleza maono ya kujenga Hospitali mpya ya kibingwa ama kuiongezea uwezo Hospitali ya Mkoa ya Mount Meru ili kukidhi viwango vinavyohitajika Kimataifa.



Aidha wawili hao Katika mazungumzo yao leo Januari 10, 2025, wamekubaliana kuendelea kushirikiana katika kutimiza dhamira ya Rais Samia katika kuwapatia wananchi huduma bora za kiafya, ambapo Waziri Mhagama amesema Wizara yake pia ipo mbioni kuupatia Mkoa wa Arusha mashine mpya ya MRI kama sehemu ya maboresho ya utoaji wa huduma za kiafya Mkoani hapa na kuondokana na changamoto ya ukosefu wa mashine hiyo muhimu kwa matibabu mbalimbali.


Announcements

  • TAZAMA MATOKEO YA MTIHANI WA MOCK MKOA DARASA LA SABA 1 July 06, 2023
  • MATOKEO YA MOCK MKOA DARASA LA SABA 2 July 07, 2023
  • TAZAMA MATOKEO YA MOCK MKOA KIDATO CHA NNE July 07, 2023
  • View All

Latest News

  • RC MAKONDA ASHUHUDIA UTIAJI SAINI UJENZI WA BARABARA YA ESO - LONGDON NA UKUMBI WA MIKUTANO ARUSHA.

    April 03, 2025
  • RC MAKONDA ATAKA KUPEWA MAJINA YA WATENDAJI WANAOCHOCHEA MIGOGORO YA KIJAMII.

    March 28, 2025
  • KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA NI MAONO NA MAELEKEZO YA RAIS SAMIA- WAZIRI NDUMBARO.

    March 28, 2025
  • OFISI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI YAFANYIA KAZI MALALAMIKO WANANCHI WA MIANZINI ARUSHA.

    March 28, 2025
  • View All

Video

UZINDUZI WA BARABARA YA WASO-SALE
More Videos

Quick Links

  • Guildlines Towards the use of ICT In Government
  • SALARY SLIP
  • Taarifa ya Mapato
  • Taarifa za Shule (SIS)
  • Takwimu za Sekta ya Elimu (BEMIS)
  • Video

Related Links

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Public Servant Portal
  • Takwimu
  • TANAPA

World visitors tracker

world map hits counter

Contact Us

Other Contacts

   

Visitors Counter

writingMasterThesis

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Sitemap
    • FAQ

Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.