Mkoa wa Arusha ukiiwakilisha nchi ya Tanzania, Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla imeweka rekodi ya Dunia kwa kuwa na Paredi yenye msululu mrefu wa magari 1,032 aina ya Landrove, kwenye LandRober Festival 2024, iliyofanyika Leo Jumamosi Oktoba 12, 2024.
Akitangaza rekodi hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda ameweka wazi kuwa, Mkoa huo wa Kaskazini mwa Tanzania, umefanikiwa kuvunja rekodi ya Ujerumani iliyowekwa mwaka 2018, kwa Taifa hilo kufanikiwa kuwa na Tamasha lililokutanisha magari chapa ya Land Rover ya kuwa na magari 1,032.
Tamasha la Land Rover Festival 2024 lililoanza mapema leo Oktoba 12 na kutarajiwa kufikia tamati Oktoba 14, 2024 limefanikiwa kushirikisha magari chapa ya Land Rover takribani 1034, na kuweka rekodi ya kuwa na Parade ndefu zaidi duniani yenye zaidi ya Kilomita 14 ikianzia safari yake Eneo la King'ori na kutamatikia kwenye viwanja vya Magereza Kisongo Jijini Arusha.
Land Rover Festival 2024 inafanyika kwa mara ya kwanza Mkoani Arusha na Tanzania, ikiwa na lengo la kuutangaza utalii wa Mkoa wa Arusha pamoja na kufungua fursa mbalimbali za kiuchumi kwa wakazi wa Mkoa wa Arusha kwa kuwa na matukio mbalimbali yatakayokusanya idadi kubwa ya watu na hivyo kuchangia kukuza pato la mwananchi mmoja mmoja na la Mkoa kwa Ujumla.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.