Wanafunzi kutoka jamii ya wafugaji wilaya ya Longido, wamejiunga na kidato cha kwanza kwenye shule mpya ya Sekondari Sinya, shule iliyojengwa na Serikali ya awamu ya sita kwa gharama ya shilingi milioni 570 kupitia mradi wa kuboresha mindombinu ya elimu ya sekondari (SEQUIP).
Shule hiyo iliyojengwa ndani ya kata yao, licha ya kuwapunguzia mwendo wa kutembea umbali mrefu, imeongeza usalama wao kutokana na sehemu ya kata hiyo kuwa ni shoroba ya wanyama pori, iliyohatarisha maisha yao pia.
Hata hivyo wajumbe wa Kamati ya Siasa Mkoa wa Arusha wametembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa shule hiyo mpya na kuipongeza juhudi za Serikali ya awamu ya sita, kwa kutekeleza Ilani ya Chama cha Mapinduzi kwa vitendo, iliyolenga kuborehsa miundombinu ya elimu ili kutoa fursa kwa watoto wote wa kitanzania kupata elimu bila malipo.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.