Katibu Tawala Msaidizi mipango bwana Said Mabie amefurahishwa na asasi zisizo za Serikali zinavyojikita katika utoaji elimu juu ya mikopo ya asilimia 10 inatolewa na Serikali.
Amesema hayo alipokuwa akifungua kikao cha wadau wanaofadhiliwa na taasisi ya Foundation for Civil society (FCS) na Viongozi wa Mkoa wa Arusha.
Bwana Mabie amesema amefurahishwa na asasi hizo zinavyofanya kazi karibu na Serikali kwa lengo la kuleta maendeleo ya Mkoa.
Aidha, bwana Mabie amezitaka asasi hizo kuendelea kushirikiana na wataalamu wa Serikali hasa katika kutatua changamoto zilizopo kwenye Jamii.
Katika kikao hicho maazimio mbalimbali yaliwekwa ikiwemo kuhakikisha ushirikiano unaendelea kuwepo baina ya sekta binafsi na Serikali ili changamoto ziweze kubainika na kutatuliwa katika Jamii.
Kikao hicho kilijumuisha asasi zisizo za Kiserikali CWCD, Okoa New Generation, Hakikazi Catalyst, Mwedo, Voice for Youth, fcs pamoja na watalaamu mbalimbali kutoka Serikalini.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.