Baba Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania - Dayosisi ya Kaskazini Kati Dkt. Solomon Jacob Massangwa amestaafishwa kwa heshima, baada ya kuhudumu katika Kanisani hilo kwa miaka 42.
Ibaada maalum ya kumstaafisha Askofu Dkt Massangwa imefanyika kanisa la KKT Usharika wa Kimandolu, Jumapili ya leo Septemba 29, 2024 Jijini Arusha.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda ameshiriki ibada hiyo huku Usharika wa Kimandolu Mkoani Arusha ukimshukuru na kumtaja Askofu Solomon kwa kuhamasisha kulipa madeni ya kanisa, Kuongeza fursa za elimu kwa wachungaji wapya, Kuboresha ibada kwa Kuongeza wataalamu wa Muziki kwenye Dayosisi na kuongeza uinjilishaji kwenye majimbo ya Maasai kusini na Kaskazini.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.