Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. John Mongella amekutana na kufanya mazungumzo na kamati ya Bunge ya Bajeti.
Mhe. Mongella ameiyomba kamati hiyo kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Mkoa hasa katika kufufua sekta ya Kilimo cha Mbogamboga, ili kukuza uchumi wa Mkoa.
Kamati ya Bunge ya Bajeti ipo katika ziara ya kikazi kwa siku 4 katika Mkoa wa Arusha, ambapo itatembelea maeneo mbalimbali ikiwemo mashamba ya Maua, Mbogamboga na Matunda.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.