Makamu wa Rais Dkt.Philip Isdori Mpango ameielekeza Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi kuanza mchakato wa ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami kwa kilometa 39 kutoka Engaresero wilayani Ngorongoro hadi Engaruka wilayani Monduli Mkoani Arusha ambacho kina changamoto kubwa kutokana na eneo hilo kupitiwa na safu za milima na bonde la ufa.
Dkt Mipango ametoa maagizo hayo wakati akizindua awamu ya kwanza ya ujenzi wa kipande cha barabara cha kilometa 49 kati ya Waso mpaka Sale katika barabara hiyo ya Loliondo hadi Mto wa Mbu yenye urefu wa Kilometa 217.
Barabara hiyo ya Loliondo wilaya ya Ngorongoro mpaka Mto wa Mbu wilaya ya Monduli ujenzi wake utatekelezwa kwa awamu nne.
Nae,Naibu waziri wa Ujenzi na Uchukuzi mhandisi Godfrey Kasekenya ametaja mikakati ya ujenzi wa barabara hiyo ya Loliondo hadi Mto wa mbu ambayo itafanyika kwa hatua na kwakuanza barabara yenye kilometa 49 imeshakamilika.
Dkt. Mpango amezindua barabara hiyo ya kilometa 49 ikiwa ni barabara ya kwa yenye kiwango cha lami katika Wilaya ya Ngorongoro tokea nchi ya Tanzania imepata uhuru.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.