Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Bw. Abdulmajid Nsekela amekabidhi Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda jumla ya Pikipiki 20, kufuatia kanuni za benki hiyo za kurudisha asilimia 01 ya pato faida yake kwa Jamii.
Nsekela ameweka wazi kuwa, Benki ya CRDB inashirikiana na Serikali ya Mkoa katika kuimarisha ulinzi na usalama mkoani huo.
Amesema kuwa, Benki ya CRDB inatarajiwa kufanya Mkutano Mkuu wa wanahisa tarehe 17,05,2024 mkoani Arusha, ukitanguliwa na Semina ya Wanahaisa terehe Mei 17, 2024 huku Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, akitarajiwa kuwa mgeni rasmi.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.