• Complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Arusha Regional

The United Republic of Tanzania President Office Regional Administration and Local Government Arusha Regional

  • Home
  • About Us
    • History
      • Chimbuko/Asili ya eneo
      • Orodha ya wakuu wa mikoa waliopita-Arusha
    • Dira na dhima
    • The basics
    • Strategies
  • Administration
    • Structure
    • Departments
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji Mali
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Maji
    • Units
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
  • District
    • Arusha
      • Historia
      • Viongozi
    • Arumeru
      • Historia
      • Viongozi
    • Monduli
      • Historia
      • Viongozi
    • Karatu
      • Historia
      • Viongozi
    • Longido
      • Historia
      • Viongozi
    • Ngorongoro
      • Historia
      • Viongozi
  • Councils
    • Arusha CC
    • Arusha DC
    • Meru DC
    • Monduli DC
    • Karatu DC
    • Longido DC
    • Ngorongoro DC
  • Investment Opportunities
    • Tourism
    • Livestock
    • Agricultre
    • Industrial
  • Our Service
    • Health
    • Education
    • Water
    • Land
    • Tourism
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Acts
    • Application Forms
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
    • Speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events

BOOST YAONGEZA IDADI YA WANAFUNZI DARASA LA AWALI NA LA KWANZA SHULE MPYA YA MSINGI EMAIYANI - OLDONYOSAMBU

Posted on: February 7th, 2024


Na Elinipa Lupembe 


Mradi wa Kuboresha upatikanaji wa Fursa sawa katika Ujifunzaji Bora kwa elimu ya awali na Msingi Tanzania Bara (BOOST), umewezesha, ongezeko la idadi ya wanafunzi walioandikishwa kuanza darasa la awali na darasa la kwanza shule mpya ya msingi Emayan, kijiji cha Lemanda Kata ya Oldonyosambu, wilaya ya Arumeru, iliyojengwa na Serikali kwa gharama ya shilingi milioni 348.


Mwalimu Mkuu wa shule hiyo mpya, Mwl. Moi Msilu, amethibitisha kuwa na idadi kubwa ya wanafunzi wa darasa la awali na la kwanza inayofikia wanafunzi 373 walioandikishwa kuanza shule mwaka mwaka wa masomo ulioanza rasmi Januari 08, 2024.


Amesema kuwa, uwepo wa shule katika kijiji cha Lemanda, umeongeza hamasa kwa wazazi kuwaandikisha watoto kuanza shule, tofauti na miaka ya nyuma wazazi waliwachelesha watoto kuanza shule kutokana na umbali iliyowalazimu kwenda shule ya Msingi Oldonyosambu, ambako mtoto alilazimika kutembea Km 6 mpaka 8 kwenda na kurudi shuleni kila siku.


"Kwa sasa shule ina jumla ya wanafunzi 668 kati ya hao, wanafunzi 373 ni wa darasa la awali na la kwanza sawa na asilimia 56 huku darasa la pili mpaka la saba wakiwa 295 sawa na asilimia 44, utagundua  uandikishwaji umeongezeka sana kutokana na mwamko wa wazazi uliosukumwa na shule kuwa jirani nao" Ameweka wazi Mwl. Msilu 


Hata hivyo Mwenyekiti wa Kijiji cha Lemanda Mhe. Mosses Ngalima, amesema kuwa,  uwepo wa shule karibu, umewapa fursa watoto wengi kupata elimu, tofauti na hapo awali licha ya wazazi kushindwa kuwaandikisha watoto shule kwa wakati, wapo watoto walizembea kufika shule kwa kujificha na kusababisha utoro na wapo walioacha shule, kutoka na umbali wa mahali shule ilipokuwa.


"Uwepo shule kijijini hapa, umewapunguzia watoto mwendo, hakuna mtoto anayetembea zaidi ya Km mbili kwenda na kurudi shuleni, watoto wanasoma vizuri na asilimia kubwa wanafika shule kwa wakati, tunamshukuru Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hasaan kwa kutujali sisi jamii yawafugaji, jamii imehamasika kila mzazi sasa anamruhusu mtoto wake kwenda shule kwa amani" Amesema Mhe.  


Ameongeza kuwa, wanaamini Serikali imetumia fedha nyingi sana kutekeleza mradi huo, lakini kipekee wananchi wa Lemanda wamenufaika sana, watoto wao wamepata fursa ya kupataelimu, fursa ambayo baadhi ya watoto waliikosa kwa kupelekwa kuchunga ng'ombe na wengine kuozeshwa katika umri mdogo.


Hata hivyo wanafunzi wa shuleni hapo wameishukuru Serikali kwa kujenga shule kijiji kwao na kumuahidi Mhe. Rais Mama Samia, kusoma kwa bidii mpaka vyuo vikuu na hatimaye kuzifikia ndoto zao za kitaaluma.


Obadia Philipo darasa la V, mwenye ndoto ya kuwa Daktari, amemshukuru Mama Samia, na kumuahidi kusoma kwa bidii kwa kuwa shule ina majengo mazuri ya kisasa,  walimu wanawafundisha vizuri.


"Tunamshukuru mama Samia, kwa kutujengea shule ambayo imasababisha sisi wasichana wa kimaasai kupata nafasi ya kusoma,  tunamuombea Mwenyenzi Mungu aishi maisha marefu"



#arushafursalukuki 




                        
                       
                        </div>
                        <!-- /.right-sidebar-content -->
                        <!--/END RIGHT SIDEBAR CONTENTE SECTION-->
                    </div>



<div class=

Announcements

  • TAZAMA MATOKEO YA MTIHANI WA MOCK MKOA DARASA LA SABA 1 July 06, 2023
  • MATOKEO YA MOCK MKOA DARASA LA SABA 2 July 07, 2023
  • TAZAMA MATOKEO YA MOCK MKOA KIDATO CHA NNE July 07, 2023
  • View All

Latest News

  • RC MAKONDA ASHUHUDIA UTIAJI SAINI UJENZI WA BARABARA YA ESO - LONGDON NA UKUMBI WA MIKUTANO ARUSHA.

    April 03, 2025
  • RC MAKONDA ATAKA KUPEWA MAJINA YA WATENDAJI WANAOCHOCHEA MIGOGORO YA KIJAMII.

    March 28, 2025
  • KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA NI MAONO NA MAELEKEZO YA RAIS SAMIA- WAZIRI NDUMBARO.

    March 28, 2025
  • OFISI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI YAFANYIA KAZI MALALAMIKO WANANCHI WA MIANZINI ARUSHA.

    March 28, 2025
  • View All

Video

UZINDUZI WA BARABARA YA WASO-SALE
More Videos

Quick Links

  • Guildlines Towards the use of ICT In Government
  • SALARY SLIP
  • Taarifa ya Mapato
  • Taarifa za Shule (SIS)
  • Takwimu za Sekta ya Elimu (BEMIS)
  • Video

Related Links

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Public Servant Portal
  • Takwimu
  • TANAPA

World visitors tracker

world map hits counter

Contact Us

Other Contacts

   

Visitors Counter

writingMasterThesis

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Sitemap
    • FAQ

Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.