Mbunge wa viti maalumu Mkoa wa Arusha Mheshimiwa Catherine Magige ametoa msaada wa Kompyuta 15 na Printa 3 vyenye dhamani ya shilingi milioni 33 kwa shule 3 za Mkoa wa Arusha ambazo ni Nanja, Engarenaiboir na Makiba.
Akikabidhi vifaa hivyo kwa niaba ya Mbunge huyo bwana Filipo Hamo amesema,vifaa hivyo viende kutumika katika malengo husika ili kuongeza ufanisi zaidi katika sekta ya elimu
Muwakilishi wa Mbunge Catherine Magige bwana Filipo Hamo (wa kwanza kulia) akimkabidhi Kompyuta
Kaimu Katibu Tawala bwana David Lyamongi kama msaada kwa baadhi ya shule za Mkoa wa Arusha.
Bwana Hamo amesema, ofisi ya Mbunge imekuwa ikitoa misaada mbalimbali katika jamii ili kusaidia kuleta maendeleo mbalimbali na bado itaendelea kutoa misaada hiyo.
Akipokea misaada hiyo kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Arusha David Lyamongi amemshukuru Muheshimiwa Magige kwa msaada huo kwani Serikali ya Mkoa imeweka kipaombele cha maedeleo kwenye elimu kwa kuhakikisha elimu bora inatolewa.
Pia, amewataka walimu wakuu wa shule hizi kuhakikisha wanazitumia kwa lengo husika ikiwemo kufundishia kwa kuweka mifumo ya kufundishia au wanafunzi wakazitumie katika kutafuta masomo mbalimbali kwenye mtandao.
Amesema Dunia ipo katika wakati wa matumizi makubwa ya mifumo ya mawasiliano kwa mitandao (TEHAMA) hivyo na Mkoa wa Arusha hauko nyuma katika kuhakikisha shule zote zinatumia mfumo huo ili kuwa mbale katika kuleta ufanisi.
Nae,Mkurungezi Mtendaji halmashauri ya Meru Emmanuel Mkongo, amemshukuru Mheshimiwa Magige kwa niaba ya wakurugenzi wenzake wa halmashauri ya Longido na Monduli kwa kuchagua halmashauri hizo kuwa miongoni mwa halmashauri za kupatiwa msaada huo.
Ameahidi kuhakikisha watazisimamia kwa umakini vifaa hivyo ili viweze kutumika katika malengo husika na kuhakikisha shule husika kuanza kutumia mfumo wa mtandao wa mawasiliano ili kwendana na kasi ya maendeleo ya dunia.
Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Meru bwana Emmanueli Mkongo akitoa neno la shukrani kwa muwakilishi wa Mbunge
Catherine Magige bwana Filipo Hamo kwa niaba ya wakurugenzi wengine wa halmashauri ya Longido na Monduli kwa kupatia
msaada wa Kompyuta na Printa katika shule zao.
Ofisi ya Mheshiwa Magige imekuwa ikitoa misaada ya vifaa mbalimbali katika sekta za afya na elimu katika mkoa wa Arusha kwa lengo la kuisadia Serikali katika kuleta maendeleo kwa jamii.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.