"Makadilio ya bajeti ya Afya dunia inakadiliwa kuwa Bilioni 4.65 sawa na asilimia 11% ya bajeti yote itatumika kutibu magonjwa yasiyoambukiza".
Takwimu hizo zimetolewa na Waziri wa Afya, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Dorothy Gwajima alipokuwa akifunga kilele cha maadhimisho ya Kitaifa ya wiki ya magonjwa yasiyoambukiza katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Jijini Arusha.
Amesema watanzania wasipochukua hatua za haraka za namna ya kujinga na magonjwa yasiyoambukiza kwa mujibu wa taarifa ya shirika la maendeleo duniani ya 2011/2025 inakadiliwa kuwa trilioni 7 itatumika kama gharama za matibabu ya magonjwa hayo kwa nchi zenye uchumi wa kati na chini na Tanzania ikiiwemo.
Ametoa wito kwa watanzania kuchukua tahadhari zote za kukabuliana na magonjwa hayo ili kuokoa kiasi hicho cha fedha kinachotarajiwa kutumika na badala yake fedha hiyo inaweza kwenda kutumika katika mambo mengine ya maendeleo.
Taarifa ya shirika la Afya duniani (WHO) ya 2016 imeeleza kuwa takribani 33% ya vifo vinavyotokana na magonjwa hutokea kila mwaka na hadi sasa ni 40% ya vifo kwa baadhi ya maeneo hapa Tanzania.
Ambapo dolla trilioni 47 zimeshatumika katika matibabu ya magonjwa yasiyoambukiza kwa mujibu wa taarifa ya shirika la maendeleo duniani ya mwaka 2013.
Dkt. Gwajima amesema, kutokana na katwimu hizi ni dhahiri kuwa bado juhudi kubwa zinaitajika kuchukuliwa kwa nchi yetu na Wizara imeshaanza kutoa elimu kwa jamii kupitia maadhimisho kama hayo ili kuwahakikishia watu wote wanapata uwele na kubadili tabia.
Amesisitiza zaidi ulaji wa vyakula vya asili kama vile Mbogamboga na Matunda kulingana na kipato cha mtu, kufanya mazoezi na kupima afya mara kwa mara kama njia za kuweza kudhibiti magonjwa hayo.
Nae, Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI anaeshughulikia Afya Dkt. Grace Magembe amesisitiza zaidi kuwa magonjwa hayo ya Kisukari, Shinikizo la juu la damu, Kansa Macho na mengine mengi huwa yanaanza kimya kimya katika mwili wa binadamu na yanapojitokeza ni muhimu kuanza matibabu haraka.
Aidha, amesema TAMISEMI itaendelea kuzisisitiza Mikoa na Halmashauri kutoa elimu ya kutosha kwa wananchi ili wapate uwelewa zaidi wa magonjwa haya.
Amewataka viongozi wa Mkoa na Halmashauri waendelee kutoa wito kwa wananchi kuacha uvivu ili wanapofanya kazi kwa bidii inakuwa ni njia moja wapo ya kuepuka tabia bwete ( kukaa bila kujishughulisha) na watakuwa wanajikinga na magonjwa yasiyoambukiza.
Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. John Mongella, bwana Hargeney Chitukulo amesema kati ya watu wanne ni mmoja tu ndio anaishi na tabia bwete na 30% ya watu wasiojishughulisha hufa.
Watu wengi wamesahau kula vyakula vya asili na kutofanya mazoezi ndio tabia zinazopelekea kuwa na magonjwa yasiyoambukiza.
Maadhimisho yaho yanafanyika kila mwaka na mwaka huu 2021 yamefanyika Mkoani Arusha kuanzia Novemba 6 hadi Novemba 13 na shughuli mbalimbali zilifanyika ikiwemo utoaji wa chanjo ya UVIKO 19 na watu takribani 173 wamepata chanjo hiyo ndani ya siku hizo za maadhimisho.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.