Kaim Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Nurdini Babu akimkabidhi Mwenge wa Uhuru Mkuu wilaya ya Arumeru Mhe. Emmanuela Kaganda tayari kwa kuukimbiza kwenye halmashauri mbili za Arusha na Meru kwa kuanza na Halmashauri ya Meru leo Julai 19, 2024.
Ukiwa Wilaya ya Meru, Mwenge wa Uhuru utakimbizwa umbali wa Km 242.1 na kupitia miradi 19 yenye tamanai Bilioni 17.4
Aidha katika halmashauri ya Meru Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru utakimbizwa umbali wa KM 95.6 na kukagua miradi 9 yenye thamani ya shillingi Bilioni 8.38.
Ameeleza kuwa, Mwenge wa Uhuru pia utazindua Mradi wa Ujenzi wa Box Kalavati barabara ya Mbuguni wenye thamani ya shilingi milioni 99.4, kuweka Jiwe la Msingi Kituo Cha Malezi ya watoto Cha St. Mary's Children's chenye thamani ya shilingi milioni 950, kuweka Jiwe la Msingi Ujenzi wa zahanati ya Kijamii ya DASHIR chenye thamni ya shilingi milioni 800 na kutembelea Utunzaji Mazingira na Utalii wa Nyuki Katika Hifadhi ya Misitu Ziwa Duluti, wenye thamani yake ni shilingi milioni 1. 6.
Aidha Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru, atatembelea Kikundi cha Vijana Golden Hearts, kinachojishughulisha na Usindikaji wa Asali, wenye thamani ya shilingi milino 12, ataweka Jiwe la Msingi Mradi wa Maji Patandi wenye thamani ya shilingi Bilioni 3.1, kuweka Jiwe la Msingi Ujenzi wa Shule ya sekondari Madiira Seela Sing'isi mradi wenye thamni ya shilingi milioni 624.2 pamoja na Kutembelea Chuo cha Wenye Ulemavu Usa River.
Hata hivyo atatembelea Miradi iliyowekwa Jiwe la Msingi mwaka 2023 na kutembelea Jengo la Kituo Cha Mafunzo kwa Jamii cha The Foundation for Tommorow (TFFT) Usa River - lenye tahamani ya shilingi Bilioni 2.7.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.