Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe. Felician Gasper Mtahengerwa ameongoza washiriki zaidi ya 500 wa Land Rover festival 2024 kwenye zoezi la Upandaji wa miti zaidi ya 500 kwenye Eneo la Magereza Kisongo Jijini Arusha ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Kumbukizi ya miaka 25 ya Kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Akizungumza na Wanahabari mara baada ya zoezi hilo kukamilika, Mhe. Mtahengerwa ameeleza kuwa siku tatu za Tamasha hilo la Land Rover limekuwa na athari chanya kwenye uchumi wa Mkoa wa Arusha hasa kwa wajasiriamali wadogo na wafanyabiashara mbalimbali kutokana na ugeni wa watu zaidi ya 3000 walioshiriki kwenye Tamasha hilo ambao wamekuwa wakitumia fedha zao kwenye manunuzi na matanuzi.
Miti iliyopandwa mapema leo kulingana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha ni miti ya Matunda, Vivuli na miti ya mbao ikihusisha miti aina ya Jacaranda Memosifatia, Gravilea robusta, Acrocapus, Mijohoro, Mdodoma, limao, Parachichi pamoja na Mijohoro nyekundu.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.