Mkuu wa wilaya ya Longido, Mhe.Marco Ng'umbi, amewaaribisha wageni na Wakaguzi wa Ndani Afrika, wanaoshiriki Mkutano wa 10 wa Shirikisho la Taasisi za Wakuguzi wa Ndani Afrika, unafanyika kwenye Kituo cha Mikutano ya Kilataifa Arusha (AICC) Aprili 17, 2024.
Akitoa salam za Mkoa, kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. Ng'umbi amewata wageni na watalamu hao kufurahia uwepo wao Arusha, kutoakana na uzuri wa mji huo, wenye hali nzuri ya hewa iliyozungukwa na vivutio vingi vya Utalii.
Amewashukuru wajumbe wote kwa kuchagua Arusha, kufanyika Mkutano huo muhimu, uliowakutanisha zaidi ya watalamu 1,500 wa Ukaguzi wa Ndani Afrika kutoka zaidi ya nchi 30 za Afrika, mkutano ambao unategemea kuimarisha hali ya matumizi sahihi ya rasilimali za Umma kwa nchi husika pamoja na kuboresha maisha ya watu.
"Ninawashukuru na kuwapongeza kwa kuichagua Arusha kufanya mkutano huu muhimu kwa nchi zetu za Afrika, ninawaalika kutumia fursa hii ya mkutano, kutembelea vivutio vya utalii vilivyopo Arusha ikiwemo mbuga za wanyama ili kujionea uzuri wa Uoto wa asili ili kufurahia zaidi kuwepo Tanzania"Amebainisha Mhe.Ng'umbi
Aidha, amesisitiza kuwa, Mkoa unatambua umuhimu wa Mkutano huo kwa nchi zote za Afrika, mkutano ambao umewakutanisha watalamu kwa lengo la kubadilishana uzoefu, kujifunza mbinu mpya zinazoendana na maendeleo ya kiteknolojia utakatoa mabadiliko chanya kwa Watalamu wa Ukaguzi wa Ndani Afrika.
Awali, Mhe.Ng'umbi amewahakikishi amani, ulinzi na usama kwa muda wote watakaokuwa Arusha ili kufikia malengo ya mkutano huo kwa maendeleo ya nchi zoye za Afrika kwa ujumla wake
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha, inaahidi kuwahakikisha amani, ulinzi na usalama kwa muda wote watakao kuwa Arusha, na kuongeza kuku
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.