Na Elinipa Lupembe.
Mkuu wa wilaya ya Longido Mhe. Marco Ng'umbi amesema kuwa, hali ya wilaya ya Longido kwa sasa ni shwari, hali inayoruhusu wananchi wake kujikita zaidi kwenye shughuli za kiuchumi na kijamii zinazoongeza hali ya uzalishaji mali walayani humo.
Akizungumza wakati wa mkutano na Mkuu wa mkoa wa Arusha mara baada ya kuwasili wilayani hapo, Mhe. Ng'umbi amethibitisha hali ya utulivu katika wilaya hiyo, huku wananchi wake wakiwa msatri wa mbele kulitumikia Taifa lao.
Ameongeza kuwa, viongozi na watalamu nao wanaendelea vema kutekeleza majukumu yao, kwa kusimamia shughuli zote hususani katika usimamizi wa miradi ya maendeleo kisekta, huku wakiwa mstari wa mbele kutekeleza Ilani ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka 2020 - 2025.
Mhe. Ng'umbi ameweka wazi kuwa serikali imetoa fedha za kutekeleza miradi ya elimu msingi na sekondari ikiwa ni pamoja na ujenzi wa shule mpya za sekondari wasichana, kwa gahrama ya bilioni 3, ujenzi wa mabweni mawili ya wavulana na uzio shule ya sekondari Longido pamoja na ujenzi wa shule mpya ya sekondari Kamweni Mirasi na zote ziko katika hatua nzuri za utekelezaji.
Kwa upande wa miundombinu ya barabara, ameweka wazi kuwa barabara kuu zote zinapitika kwa kipindi chote cha mwaka licha ya changamoto zinazojitokeza kutokana na mvua zinazoendelea lakini TANROAD NA TARURA, wanaendelea kufanya matengenezo ya muda maalum pamoja na kuchunguza maeneo hatarishi na kuyafanyia kazi kwa wakati.
Hata hivyo upande wa Umeme, vijiji vyote vya wilaya ya Longido vimefikiwa na miundombinu ya umeme na serikali kuendelea na kasi ya kufikisha umeme kwenye vitongoji na hatimaye kuwafikia wateja wa nyumba kwa nyumba.
Aidha, huduma za afya zinaendela kuimarika, zahanati zimejengwa kwenye maeneo ya pembezoni huku kituo cha afya cha Ngarnaiboru na Longido vyote vinatoa huduma za afya kwa wananchi huku Serikali ikileta dawa na vifaa tiba pamoja na wahudumu wa afya katika vituo vyote vya kutolea huduma za afya na kuongeza kuwa ifikapo 2025, hali ya utoaji wa huduma itakuwa imeimarika zaidi.
Awali ameweka wazi kuwa, huduma ya maji vijijini nazo zinaendelea kuimarika licha ya kuwa bado kuna changamoto kwa baadhi ya miradi ikiwemo mradi wa Tinga tinga na Ngeleani, mi4adi amabyo mkandarasi anasuasua na mpaka sasa ametuchelewesha kwa zaidi ya miezi 6 jambo ambalo litasababisha mradi huo kushindwa kukamilika mwezi Aprili kamailivyokusudiwa.
Hata hivyo ametumia wasaa huo kuishukuru serikali ya awamu ya sita chini ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kaiz kubwa anayoifanya ya kuhakikisha huduma za jamii licha ya kuimarika zinawafikia wananchi katika maeneo yao.
"Wilaya ya Longido ni moja ya wilaya za pembezoni mwa nchi, serikali ya awamu ya sita imetoa fedha nyingi za kutekeleza mirafi kisekta, miradi ambayo imewafikia na kuwanufaisha wananchi ambao hapo awali walionekana kutelekezwa, kwa sasa Longido ni shwari, kila mwanaLongido anajisikia na yeye ni Mtanzania halali" Amebainisha Mhe. Ng'umbi.
#ArushaFursaLukuki
#KaziInaendelea
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.