Tarehe 21.03.2024 Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) Kanda ya Kaskazini imetoa elimu juu ya madhara ya matumizi na usafirishaji wa dawa za kulevya na kemikali bashirifu kwa Maafisa 33 wa Mpaka wa OSBP Namanga.
Maafisa hao kutoka Taasisi mbalimbali 19 za Serikali waliopatiwa mafunzo ni kutoka Jeshi la Polisi, Uhamiaji, Zimamoto, TFS, TMDA, TRA, CED, TAEC, Mifugo, TPHPA, UM, TBS, FISHERIES na CFA
Katika mafunzo hayo Maafisa hao walioneshwa sampuli mbalimbali za dawa za kulevya na jinsi ya kuzitambua dawa za kulevya pomoja na mbinu zinazotumika kuficha dawa za kulevya.
Elimu ya madhara na tatizo la dawa za kulevya, udhibiti wa usafirishaji wa dawa za kulevya na kemikali bashirifu mipakani pamoja na sheria ya kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya itakuwa chachu ya kuimarisha mapambano dhidi ya tatizo la dawa za kulevya katika maeneo ya mipakani hususani Mpaka wa OSBP Namanga.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.