Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Arusha, Seleman Hamis Msumi, akiwasilisha taarifa fupi ya mradi wa upanuzi wa Hospitali ya wilaya ya Arusha Olturulet, mbele ya Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kudumu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), kwenye kikao kifupi kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha leo Machi 13, 2024.
Mkurugenzi Msumi ameielezea Kamati kuwa, halmashauri ya Arusha, imepokea fedha kiasi cha shilingi milioni 900 kutoka Serikali Kuu, kwa ajili ya upanuzi wa Hospitali ya wilaya ya Olturumet, kwa ajili ya upanuzi wa hospitali hiyo na tayari utekelezaji wa mradi huo umeanza na unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi Aprili, 2024.
Amesema kuwa kiasi hicho cha fedha kitajumuisha ujenzi wa majengo manne, ikiwemo jengo la wagonjwa wa nje (OPD), jengo maabara, jengo la mionzi, pamoja na ujenzi wa jengo la kuhifadhia maiti (mochwari)
Wajumbe hao wa Kamati, wakiongoza na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Denis Lazaro Londo (MB), wako mkoani Arusha kwa ziara ya siku moja ya kukagua utekelezaji wa miradi ya Maendeleo halmashauri ya Arusha, Meru na Longido.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.